February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIMETIMIA SIKU 53 TANGU VIJANA WATANO WAPOTEE DAR.

Mama mzazi wa Tawfiq Mohammed,moja ya vijana watano waliopotea tangu Disemba 26,2021,amekanusha kauli ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Jumanne Muliro,aliyedai kuwa Polisi wanashirikiana na Familia za vijana hao katika kuwatafuta.Ameongeza kuwa,wazazi wameendelea kuhangaika wenyewe kutafuta watoto wao hadi wamechoka na kukata tamaa.
Kauli ya Kamanda Muliro kuwa wanashirikiana na wazazi na ndugu wa vijana waliopotea katika kuwatafuta,aliitoa Jumatatu Februari 14,wakati akijibu swali la mwandishi wa Habari,aliyetaka kujua jitihada za kuwapata vijana hao zimefikia wapi.