Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),Onesmo Olengurumwa na Afisa Uchechemuzi,Lisa Kagaruki hii leo wanafanya ziara ya siku moja kwa wanachama wa mtandoa huo mkoani Shinyanga. Ziara hii itafanyika siku ya leo, Jumamosi 22 Mei 2021.
Mratibu atapata fursa ya kutembelea mashirika wanachama wa THRDC matano ambayo yapo katika mkoa wa Shinyanga ikiwemo Shirika la Rafiki Social Development Organization,Agape Aids Control Program,The Voice of Marginalized Community,Shirika la HUHESO pamoja na Shirika la Haki za Binadamu Kahama.
Dhumuni kuu la ziara hii fupi ni mtandao kufahamu kwa undani zaidi wanachama wake na kazi wazifanyazo, kujua changamoto zinazowakabili na ni kwa namna gani Mtandao unaweza kushirikiana nao kuzitatua. Ziara hiyo inalenga pia kutathmini hali ya haki za binadamu katika mkoa wa Shinyanga.
Ziara hii ni muendelezo wa ziara ambazo zimekwisha kufanyika, kanda ya mwisho kutembelewa ilikua kanda ya Kati.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.