February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA TAASISI YA VIFAFIO

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Victoria Farming and Fishing Organization (VIFAFIO) linalojishughulisha na masuala ya Uvuvi, ufugaji na Kilimo.

Taasisi ya VIFAFIO inafanya Kazi ya kutetea Haki za wavuvi, wakulima, inahamasisha utunzaji wa Mazingira kwa kupanda Miti huku ikifikia wilaya 5 za mkoa wa Mara.

Taasisi imekuwa ikifanya Kazi kwa miaka 21 Sasa, Ina wanachama 3925 huku ikifanikiwa Kuwafikia wanufaika zaidi ya 9000. Kwa mwaka 2021/2021 miradi inayoendeshwa na VIFAFIO imejikita katika utunzaji wa vyanzo vya maji na Taasisi imekuwa ikipata Ushirikiano mzuri kutoka kwa Wadau, na Serikali, wafadhili mbali mbali ambao wamekuwa wakifadhili baadhi ya miradi.

Taasisi imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo utegemezi kwa wafadhili ambao kwa kiasi kikubwa miradi ikiisha na baadhi ya shughuli husimama, hasa katika kipindi hiki Cha mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo wafadhili wengi wamekuwa wakisitisha baadhi ya miradi jambo linaloathiri utendaji wa Taasisi.

Bado taasisi ya VIFAFIO haijafanikiwa kuwahamasisha wanachama wake kulibeba Shirika na kuchangia kiasi kitakachowasaidia taasisi kusimama hata wakati ambao hakuna wafadhili.

Siasa zimekuwa zikisababisha baadhi ya wavuvi kutokuelewa wapi pa kuelekea hasa kipindi cha chaguzi ambapo wanasiasa wanakuwa namaagizo tofauti yanayobadili mitazamo ya wavuvi katika swala la utunzaji wa Mazingira.

Mratibu THRDC ameipongeza taasisi kwa kuona umuhimu wa kusimamia katika eneo la utunzaji wa Mazingira kwa Kuwa ndio Shirika linalofanyia Kazi eneo la wavuvi, eneo amba ambalo halina Wadau wengi lakini limekuwa na changamoto nyingi zinazoigusa jamii kubwa na Watanzania.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC