February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA TAASISI YA TUJIKOMBOE PARALEGAL ORGANIZATION

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Shirika la Tujikomboe Paralegal Organization lililopo Wilayani Tarime mkoani Mara.

Tujikomboe ni taasisi inayojishughulisha na utoaji wa msaada wa kisheria, utoaji wa Elimu ya Haki za Binadamu, uhamasishaji jamii kuondokana na Mila na desturi potofu, taasisi imekuwa ikizisaidia Serikali za vijiji kuandaa kanuni za ufuatiliaji wa masuala ya ukatili wa kijinsia (GBV) hasa kwa mabinti wanaoacha shule, Pamoja na usuluhishaji wa migogoro ya ardhi kwa kushirikiana na taasisi za utetezi wa Haki za Binadamu Wilayani Tarime.

Taasisi imekuwa ikifanya uhamasishaji kwa wanaume kuandika mirathi Ili kupunguza migogoro katika familia pindi mwenza mmoja anapofariki katika familia.

Kwa kipindi cha Juni 2020 Hadi Julai 2021 taasisi imefanikiwa kuwahudumia watu 140, kusuluhisha kesi 94 na kuhamisha kesi 46.

Tujikomboe Paralegal Organization imefanikiwa kutatua na kuIpatia haki kesi 26 za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na 12 kwa watoto.

Pamoja na kazi kubwa iliyofanywa na Taasisi ya Tujikomboe Paralegal Organization Bado imekuwa ikikumbana na changamoto za kiusalama katika Utatuaji wa kesi kwenye maeneo kama ukamataji wa watuhumiwa jambo linalopelekea baadhi kutishia maisha, changamoto ya kifedha kwa taasisi inachangia baadhi ya shughuli kutofanyika kwa wakati na nyingine kutokamilika, wasaidizi wa kisheria wamekuwa wakiacha Kazi Kutokana na kutokuwa na moyo wa kujitolea kwani shughuli za Utetezi zimekuwa zikihitaji kujitoa zaidi, jamii ya watu waishio katika wilaya ya Tarime mara nyingi imekuwa ikichukua hatua za kujichukulia sheria mkononi jambo linalopelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mratibu THRDC alipata wasaha wa kukabidhi machapisho yaliyoandaliwa na Mtandao, na kuitaka taasisi kuangalia Mpango mkakati wa Miaka mitano wa maendeleo ya Taifa uliotaja maeneo ya kipaombele kwa Serikali Ili taasisi ifahu malengo ya Serikali na kuona namna inavyoweza kuchangia katika maendeleo hayo kwani Asasi za Kiraia ni Wadau muhimu wa maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC