February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA TAASISI YA MUSOMA MUNICIPAL PARALEGAL CENTRE (MMPO)

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea taasisi ya MMPO inayojishughulisha na huduma ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa Makundi ya Wanawake na watoto wanaokumbwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia.

Taasisi iliyoanza mwaka 2013 ina wasaidizi 9 wa kisheria (Paralegals) wanaosaidiana katika utoaji wa huduma ya elimu na ushauri wa kisheria, huku kesi za jinai zinazohitaji kwenda mahakamani zinapatiwa Mawakili wanaoshirikiana na Taasisi kuzisimamia kwani taasisi Bado haina uwezo wa kusimamia kesi kubwa.

Kupitia miradi mbalibali taasisi imefanikiwa kuwafikia watu 37,000 kwa huduma ya Elimu ya kisheria, 367 wamenufaika na msaada wa kisheria uliotolewa na Taasisi kw amtu mmoja mmoja na Hadi kufikia Sasa kesi 3 zinaendelea mahakamani.

Katika ufanyaji Kazi taasisi Ina mashirikiano mazuri na Serikali, jambo lililopelekea viongozi wa Kiserikali akiwemo mwenyekiti wa mtaa kutoa naafasi katika ofisi za Serikali kwa ajili ya taasisi hiyo kuendelea kujiendesha lakini pia kutoa vibali pindi taasisi inapotakiwa kutembelea mashuleni kwa ajili ya utoaji wa Elimu na msaada wa kisheria.

Taasisi ya MMPO inakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo uchache wa wafanyakazi wa kudumu wa Taasisi kwnai mfumo wa Taasisi ni wa kujitolea hivyo wasaidizi wa kisheria wanapopata sehemu zinazowapatia maslahi huacha taasisi na kuondoka.

Changamoto ya mawasiliano hasa kwa kundi la watu wenye Ulemavu katika upataji wa msaada wa kisheria. Hii ni kwa sababu taasisi Bado haijawa na uwezo mkubwa wa kuajiri wataalamu wa lugha za alama hivyo hupelekea kundi la watu wenye Ulemavu kushindwa kuwasiliana pindi wanapohitaji msaada.

Kutokuwa na fedha kwa ajili ya kuendesha miradi ya taasisi kwani mpaka sasa taasisi inategemea mfadhili mmoja tu LSF ambaye husaidia upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya ofisi hivyo miradi mikubwa inapata ugumu kufanyika.

Hata hivyo taasisi inajitahidi kujikwamua kutoka katika changamoto hizo kwa kujiunga katika mitandao kama Tanzania Paralegal Network (TAPANET) Ili kuweza kufanya Kazi kwa Umoja na kuisaidia jamii kwa Upana zaidi.

Mratibu THRDC ameipongeza taasisi ya MMPO kwa Kazi nzuri ya kuifikia jamii kubwa kwa utoaji wa msaada na elimu ya kisheria na pia ameishauri taasisi kuona umuhimu wa kujiunga na Taasisi nyingine zinazofanywa Kazi ya usaidizi wa kisheria Ili kupata fursa za kushiriki Mafunzo mbali mbali Ili Kuwa na uwezo wa kuyahudumia Makundi yote kwa weledi.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC