Na Loveness Muhagazi
Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo ametembelea taasisi ya Geitasamo Paralegal Network iliyopo kata ya Matare Wilayani Serengeti mkoani Mara.
Geitasamo Paralegal Organization ni taasisi inayojihusisha na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa eneo la Wilaya ya Serengeti, utoaji wa Elimu ya kisheria mashuleni, kuendesha mikutano na makongamano, utoaji wa Elimu ya uhifadhi maliasili, kutoa elimu ya Ujasiriamali Ili kuondoa umasikini kwa kina mama waishio katika mazingira magumu, kukusanya Taarifa za matukio ya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu kwa Jamii, pamoja na walimu Ili kuisaidia jamii kuondokana na matatizo yatokanayo na ukatili wa kijinsia.
Taasisi ya Geitasamo Paralegal inatamani kuona jamii inaheshimu na kulinda Haki za Binadamu kwa maendeleo endelevu ya Jamii.

Hata hivyo Shirika Lina malengo ya kujikomboa kutoka kwenye vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuijenga uwezo kupitia Mafunzo mbali mbali ya kisheria, utawala bora, utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria, shughuli za kujizalishia kipato Ili kuliwezesha Shirika ikiwemo kuendesha shughuli za Utoaji wa msaada wa kisheria kupitia ufugaji wa nyuki, kilimo Cha buatani, Pamoja na kilimo Cha mazao ya biashara na chakula.
Hata hivyo Kwa mwaka 2019 Shirika lilifanikiwa kuwafikia watu 75,302 kupitia elimu ya kisheria kwa kata 30, kwa mwaka 2020 watu 204,453 hii inafanya idadi ya watu 279,755 waliofikiwa kwa huduma ya Elimu wa kisheria kwa mwaka 2019/2020.

Taasisi imefanikiwa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu 262 Kwa mwaka 2019, huku watu 280 wameweza kufikiwa kwa mwaka 2020 na hii ni kwa huduma za mashauri ya Ardhi, ndoa, jinai, mirathi, madai, matunzo ya watoto, unyanyasaji, ukatili wa kijinsia, Kazi na maeneo mengine.
Taasisi imekuwa ikishirikiana na Wadau wengine katika utoaji wa huduma za utetezi wa Haki za Binadamu ikiwemo ofisi ya DED wilaya ya Serengeti, Dawati la Jinsia, Nyumba salama, Serengeti media center, hope for Girls na Taasisi nyinginezo.

Pmamoja na Kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya Geitasamo Paralegal Network Bado inakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa usafiri ambao ungeiwezesha taasisi kufikia maeneo mbali mbali ya wilaya kwa huduma mbali mbali za msaada wa kisheria, upungufu wa wasaidizi wa kisheria na wengine kujiondoa katika shughuli za utetezi, Ushirikiano mdogo kutoka kwa Jamii na watendaji wa Serikali, kutokuwa na elimu ya Mafunzo ya Usalama yanayowezesha taasisi kukabiliana na vitisho kutoka kwa Jamii.
Mratibu THRDC ameipongeza taasisi kwa Kuwa na mfumo mzuri wa utunzaji Taarifa, na kuahidi Kuwa Mtandao utaandaa mfumo mzuri wa Watetezi wa Haki Kanda ya Ziwa kupatiwa mafunzo ya kiusalama Ili kuwawezesha kufanya akazi zao kwa Usalama zaidi.
Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC
13/08/2021
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.