February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA WOTE SAWA

Hii Leo Agosti 10, 2021 Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania Onesmo Olengurumwa anaendelea na ziara ya kutembelea wanachama wa Mtandao Kanda ya Ziwa kwa mkoa wa Mwanza, ambapo ametembelea Shirika la Wote sawa linalojihusisha na masuala ya utetezi wa Haki za mabinti wasaidizi wa Kazi za ndani wanaokumbana na changamoto za ukatili wa kijinsia pindi wawapo katika maeneo ya Kazi au wanaotumikishwa kabla ya kufikia umri unaowaruhusu kufanya Kazi hizo.

Taasisi ya Wote Sawa imefanikiwa kufungua ofisi nyingine mkoa wa Kigoma katika wilaya ya Kasulu Pamoja na Ngara ambapo ofisi zote hizi zimekuwa zikifaamya Kazi ya kuwajengea uwezo mabinti wafanyakazi wa ndani kupata stadi za maisha zinazowawezesha kuinuka kiuchumi na kukata mnyororo wa umasikini lakini pia taasisi ya Wote sawa imekuwa ikiwahusiaha wasaidizi wa kisheria ‘paralegals’ kutoa elimu katika maeneo mbali mbali ikiwemo utambuzi wa Haki zao.

Taasisi ya Wote Sawa imeweza Kuwa na nyumba salama katika mikoa ya Mwanza na Kigoma ambapo kwa kituo cha Kasulu pekee mpaka Julai 2021 Jumla ya wahanga wa Ukatili 142 wameweza kusaidiwa tofauti ya idadi ya wahanga 75 iliyotarajiwa mwanzo na katika maeneo haya wahanga wamekuwa wakipatiwa huduma zote stahiki na kuwezeshwa kuwa salama, taasisi imeweza kukua zaidi na kupata wafadhili wa miradi mbali mbali, kufungua klabu 263 mashuleni, watu zaidi ya 50,000 wamesaidiwa Moja kwa Moja na Taasisi, taasisi imeweza Kuwa na mahusiano mazuri na Wadau ndani na Nje ya nchi, mashirika kama SAWAU, KIWOHEDE, Kivulini WILDAF, EMEDO nk.

“Tumekuwa tukipokea Taarifa za ukatili kutoka Serikali za mitaa, vituo vya polisi na sababu kubwa zimekuwa ni ukatili wa kingono kutoka kwa waajiri Pamoja na changamoto za mishahara.”

“Mpaka sasa tumewasaidia mabinti wawili kuweza kueudi shuleni kwa ngazi ya sekondari, tunaibua vipaji, tunatoa msaada wa mitaji, na Kwa mwaka 2021 tumeweza kuwaokoa mabinti 55 kani mpaka sasa hapa kituoni tuna mabinti 22” Deminitilia Faustine Afisa kutoka wote Sawa

Wote sawa inajengea uwezo vikundi vya mabinti wafanyakazi wa ndani katika wilaya za Nyamagana na Ilemela ambapo tayari kikundi kimoja kimeweza kuaajiliwa kisheria na kuweza kupata mikopo ya asilimia 4% ya mikopo ya vijana inayotolewa na Serikali kwa vikundi vya wafanyakazi wa Kazi za ndani, lakini pia taasisi inaendesha kampeni ya kk ibubu changu ambapo mtaalamu kutoka benki anapata muda wa kukutana na mabinti na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kuweka akiba, lakini pia kupatiwa bima ya Afya.

Pamoja na Kazi kubwa na mafanikio ya taasisi ya Wote Sawa Bado inakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo kutokuwa na idadi kamili ya Mabinti wahanga wa ukatili wa kijinsia, kuwepo kwa miradi ya muda mfupi, kutokuwepo na fedha za kutosha kusaidia katika uandishi wa ripoti mbali mbali, Ushirikiano mdogo kutoka kwa familia na jamii za wahanga kwani baadhi ya kesi humalizwa kifamilia na hata viongozi wa Serikali za mitaa, kutokuthaminiwa na kutambulika kwa wafanyakazi wa ndani na kuchukuliwa ni watu wa chini wasiohitajika kisimamiwa Haki zao, ucheleweshwaji wa kesi jambo linalopelekea mashahidi kuchoka na kughairi kutoa shahidi mahakamani, uhasama kwa watendaji wanaofuatilia kesi za ukatili kwa mabinti Pamoja na vitisho kutoka kwa Jamii hasa pale taasisi inapogusa kesi zenye maslahi ya wakiukaji wa Haki hiz.

Taasisi ya Wote Sawa inaeleza Kuwa imekuwa ikijitajidi kuepuka vhaangaamoto hizo kwa kuwatumia viongozi wa kijamii, kuhakikisha watendaji wanatoa Taarifa za kesi zote wanazofuatilia na kuepuka kufuatilia kesi hizo katika hali hatarishi.

Hata hivyo Wote Sawa kama mwanachama wa Mtandao Inakiri kupata mchango mkubwa kutoka THRDC, mchango ambao umeifanya taasisi hiyo kukua lakini pia mafunzo na fursa zinazotolewa na Mtandao yamenufaisha taasisi kwa kuiwezesha kuboresha mahusiano na Taasisi nyingine za utetezi wa Haki za Binadamu, taasisi imepata nafasi ya kupata Mafunzo ya Usalama, kama tasisi tunaaendelea kuhakikisha tunatumia Mafunzo kuboresha usamala wa Ofisi Ili kupunguza changamoto zinazoweza kusababishwa na kutokuwa salama.

Mratibu THRDC ameishauri taasisi kuendelea kuchukua tahadhari hasa Kutokana na Kazi hiyo kiKugusa maslahi ya wananchi wanaokiuka Haki za wafanyakazi wa majumbani, lakini pia ameiahauri taasisi kuwa na Sera ya Usalama na kuendelea kutoa Mafunzo ya kujilinda kwa kila mwajiriwa mpya anayejiunga na Taasisi huku akiipatia taasisi vitabu vya compliance Ili kuweza kuendaana nasera na miongozo ya Serikali katika uendeshaji wa Taasisi.