February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA WASAIDIZI WA KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU SERENGETI (WASHEHABISE)

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa akiambatana na Afisa Dawati la Wanachama Bi. Lisa Kagaruki hii Leo wametembelea ofisi za Taasisi ya WASHEHABISE zilizopo Wilayani Serengeti mkoani Mara.

WASHEHABISE ni taasisi inayojihusisha na utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa jamii ya wakazi wa Wilaya ya Serengeti na vitongoji vyake.

Taasisi ya WASHEHABISE inatoanelu Kuhusu masuala ya kisheria, imekuwa ikifundisha kuhusiana na masuala ya Haki za Binadamu, taasisi imekuwa ikiyayumia makongamano ya kiserikali kupata wasaha wa kuielimiaha Wananchi kuhusiana na masuala ya Haki za Binadamu na elimu ya sheria Nchini.

Taasisi imekuwa ikiendesha kipindi cha radio Cha kuhamasisha ulinzi wa Haki za Binadamu kwa Jamii, imeanzisha Klabu 11 mashuleni ambapo kila klabu Ina wastani wa wanafunzi 30- 50 wanaohamasishana kuhusu ulinzi wa Haki za Binadamu.

Kwa mwaka 2020 taasisi ilikuwa na wasaidizi 16 wa kisheria ambapo Jumla ya watu 70 wakipatiwa huduma ya msaada wa kisheria, mashauri 35 yalipata Rufaa, wanawake na watoto 56 wakipatiwa huduma ya msaada wa kisheria, taasisi imefanya uhamasishaji wa kuweka maji tiririka kw akila kaya Ili kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO19.

Taasisi imefanikiwa kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo utoaji wa Elimu ya Haki za Binadamu mashuleni, ambapo shule 7 zimefanikiwa kufikiwa, kutoa elimu katika mabaraza 7 yaa kata, shughuli mabazo kwa Pamoja zimechochea mwamko wa uelewa wa haki za Binadamu kwa rika tofauti.

Taasisi ya WASHEHABISE Bado inakumbana na changamoto ya usafiri kuweza kuwafikia walengwa hasa walioko katika maeneo ya pembezoni ambayo huhitaji usafiri Ili kufikiwa kwa haraka, ambapo mara kadhaa taasisi hutumia gari ya halmashauri kwa kuchangia mafuta na kuwafikia walengwa.

Taasisi Bado haijapatiwa Mafunzo ya kiusalama Ili kuiwezesha kufanya kazi zao kwa Uhuru huku wakifahamu Sheria zinazowasimamia.

Kutokuwepo na mfumo mzuri wa upokeaji wa Taarifa za matukio ya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu ambao utawezesha kupokea Taarifa kwa wakati, lakini pia katika swala la uandishi Bado taasisi haijawa na namna Bora ya uandaaji wa ripoti za Kazi zinazofanywa na Taasisi Ili kuwawezesha wafadhili kufahamu kwa undani shughuli kubwa zinazofanywa na Taasisi.

Mratibu THRDC ameahidi taasisi Kuwa Mtandao utandaa mfumo mzuri utakaokiwezesha taasisi kuandika ripoti mbali mbali, kuzielekeza taasisi namna ya kufanya ‘fundraising’ Pamoja na uandishi wa miradi Ili kuweza kupata wafadhili watakaoziwezesha taasisi kufanya Kazi kwa ufanisi zaidi na kufikia wahitaji wengi wa huduma ya msaada wa kisheria.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC