February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA WADADA SOLUTION

Na Loveness Muhagazi

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo ametembelea Shirika Mwanachama qqa mtandao liitwali Wadada Solution.

Wadada Solution ni Shirika linalojihusisha na shughuli za utetezi wa Haki za watoto na vijana Ikiwemo utoaji wa elimu ya Haki za Binadamu kwa kuendesha midahalo mashuleni, kufanya vipindi vya radio, kutoa msaada wa kisheria, Pamoja na usaidizi wa kiuchumi kwa utoaji wa mikopo bila riba kwa vijana na wasichana.

Shirika la Wadada Solution linashirikiana na Serikali kupitia ajeahi la polisi, mashirika mbali mbali ya utetezi wa haki za Binadamu ikiwemo taasisi kama Sauti ya Wanawake Ukerewe, TAWLA, TLS na Taasisi zingine hii yote ni kuhakikisha linaifikia jamii kwa upana zaidi.

Mkurugenzi wa Shirika la Wadada Solution Bi. Ruth John ameishukuru THRDC kwa kutoa usaidizi wa kisheria pindi aliposhikiliwa na Jeshi la polisi wakati wa utekelezaji wa shughuli za utetezi.

Shirika la Wadada Solution linajivunia miaka 10 ya ufanyaji Kazi za utetezi ambapo mwaka 2015 Shirika lilikuwa na mwajiriwa mmoja ukilinganisha na Sasa ambapo Shirika Limefanikiwa kuajiri wafanyakazi 10, huku likitekeleza miradi minne ya kuisaaidia jamii, huku taasisi ikishirikiana kwa ukaribu zaidi na Serikali kuifikia jamii.

Pamoja na mafanikio hayo Wadada Solution inakiri kukumbana na Changamoto mbali mbali ikiwemo usiri na kukosekana kwa Ushirikiano kutoka kwa Jamii, baadhi wafanyakazi wa taasisi kama hospitali kuharibu shahidi za ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti pindi zinapohotajika na Mamlaka kama Jeshi la polisi, Rushwa, kutokuwepo kwa Uelewa wa namna sahihi wa utunzaji wa kumbukumbu Baada ya Utekelezaji wa miradi jambo lililopelekea kushindwa kujua idadi sahihi ya wanufaika wa huduma za shirika.

Pamoja na kutokuwepo kwa takwimu sahihi za idadi kamili ya wanufaika wa Shirika la Wadada Solution, bado Mkurugenzi wa Shirika hili Bi. Ruth John anakiri Kuwa Shirika hilo limekuwa chachu kubwa ya kuwasaidia vijana na mabinti waliopo mashuleni kupata uelewa wa masuala ya Haki za Binadamu huku wengine wakishikwa mikono Moja kwa Moja na Shirika, akitolea mfano wa kijana Frank Deus Aliyepata msaada wa usaidizi wa fursa zilizomsaidia kumaliza elimu yake hasa Baada ya kuondokewa na mzazi wake, usaidizi huo umemwezesha kijana Frank kufaulu vizuri masomo yake.

Hata hivyo Mratibu THRDC ameweza kukabidhi majarida mbali mbali likiwemo jarida linalotoa mwongozo kwa wanachama juu ya namna ya kuendana na sheria za Utekelezaji wa sheria zinazosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali Pamoja na muongozo wa kupambana na Janga la UVIKO 19 na majarida mengine mengi.

MWISHO