February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA TANZANIA WOMEN LAWYERS ASSOCIATION (TAWLA)

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Shirika la Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) tawi la Mwanza.

TAWLA ni mojawapo ya mashirika ya Mtandao ambalo lilitambuliwa na kubahatika kupata Tuzo kutoka kwa mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC katika siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu Julai 2, 2021, Tuzo iliyolitambua shirika hilo kwa ufanyaji kazi mzuri katika utetezi wa Haki za wanawake Pamoja na kuiwezesha jamii kupata haki katika maeneo mbali mbali.

TAWLA imekuwa ikifanya kazi za Utoaji wa msaada wa kisheria, kusimamia kesi za ukatili wa Kijinsia (GBV) kesi za Mirathi, kesi za usimamizi wa familia (Matrimonial) kufanya usuluhishi wa baadhi ya kesi ambazo hazihitaji kwenda mahakamani ikiwemo usuluhishi wa ndoa ambazo zikishindikana hufanyiwa ‘referral’ katika mabaraza ya kata ya usuluhishi.

Pamoja na Kazi zote hizi zinazofanywa na shirika kwa mkoa wa Mwanza TAWLA inakiri kupokea kesi nyingi Zaidi katika eneo la ‘child maintenance and custody’ Matunzo na Malezi ya Watoto pindi wanandoa wanaposhindwa kuishi Pamoja hasa baada ya ndoa kuvunjika, jambo lililopelekea taasisi kuanzisha utaratibu wa kupokea fedha za matumizi kutoka kwa mwenza mmoja kuelekea kwa mwingine kwa ajili ya matunzo ya Watoto pindi wanaposhindwa kuishi Pamoja kama mume na mke.

Licha ya TAWLA kuwa kinara katika utetezi wa haki za wanawake, lakini wanufaika wengi wa huduma za taasisi hii wamekuwa wakikumbana na changamoto za kifedha jambo linalopelekea kushindikana kwa uendeshaji wa kesi, Lakini pia kumekuwa na utekelezwaji mgumu wa kesi kutokana na aina ya washtakiwa na kesi ambazo mara nyingi zimekuwa zikionekana kuwa za kifamilia Zaidi.

Mratibu THRDC ameipa Kongore taasisi hii ya TAWLA kwa kuanzisha mfumo huo ambao kwa kiasi kikubwa umeonekana kupunguza migogoro na kadhia kwa Watoto pindi wanandoa wanapoachana huku akiipatia taasisi Vijarida vya compliance (mwongozo wa mashirika yasiyo ya kiserikali) na kusisitiza kuendelea kwa kuzingatia usalama wao katika shuguli za utetezi wa haki za binadamu, pamoja na kuendelea kuzingatia sheria zinazowekwa na serikali katika usimamizi wa NGO’s .

MWISHO