February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA SAUTI YA WANAWAKE UKEREWE (SAWAU)

Na Loveness Muhagazi

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa anaendelea na ziara ya kutembelea wanachama wa Mtandao, mkoani Mwanza. Katika ziara hii iliyoanza Leo Mratibu ameanza kwa kutembelea Shirika Mwanachama la “Sauti ya Wanawake Ukerewe” ambalo pia ni Mratibu wa wanachama Kanda ya Ziwa, linalopatikana mtaa wa Kahgaye B Maduka Mawili, kata ya Nyakato, wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.

Steven Nzunda ni Afisa Programu katika Shirika la hili la SAWAU anaelezea kazi zinazofanywa na shirika ikiwa ni Pamoja na utoaji wa msaada wa kisheria, Elimu ya afya ya uzazi, uelimishaji wa mabinti waliopata mimba katika umri mdogo, kuwaelimisha mabinti kutambua Haki zao, kuwajengea uwezo paralegals Kuweza kutoa elimu katika baadhi ya maeneo kuhusu Haki za wanawake.

“Tumekuwa tukiandika miradi mingi katika usaidizi wa vijana na wasichana Pamoja na tukishirikiana na mashirika mengine katika kufanya intervention na katika mashirikiano haya tumekuwa tukigundua mashirika mengi yamejikita katika Elimu zaidi lakini katika swala la Haki hawapo ndani Sana, hivyo tukaona tujikite humo na tumewasaidia mabinti na wanawake wengi kupata Haki zao” Anaeleza Steven Nzunda, Afisa Programu kutoka Shirikap la SAWAU

Pamoja na Kazi hizi Shirika la SAWAU linajivunia Kuwa chanzo cha Tabasam kwa mabinti na wanawake wengi ambapo limeweza kuwasaidia zaidi ya mabinti 700 kwa maeneo ya wilaya ya Ukerewe na jiji la Mwanza kwani zaidi limwkuwa likiwapatia elimu za Ujasiriamali wa ushonaji, utengenezaji wa mapaambo Pamoja na uandaaji wa mkaa mbadala shughuli ambazo kwa Pamoja zimekuwa zikiwapatia kipato

Pamoja na Manufaa hayo Bado Shirika la SAWAU linakiri kukumbwa na Changamoto kadhaa ikiwa ni Pamoja na kupata ugumu kuaminika kijamii, kuwepo kwa ugumu wa kupata kibali Cha kutoa elimu ya Sexual reproductive Health.

Kupitia changamoto hizo Shirika la SAWAU limeweza kuwatumia wafanyakazi wa afya wa Jamii kusaidia kutoa elimu zaidi na kuwaelimisha watu Pamoja na kuitoa hofu jamii, Kutokana na ugumu kwenye utoaji wa maafunzo ya Elimu ya Afya SRHR (sexual reproductive health rights )Sasa Shirika la SAWAU Linatoa elimu ya kujitambua kwa Jamii Ili kuendelea kupata uelewa zaidi.

Hata hivyo Mratibu awashauri wanachama kuendelea kufuata sheria ambazo zimewekwa na Mamlaka husika katika Utekelezaji wa majukumu yao, watumie vizuri kitabu kilichochapishwa na Mtandao. Pia washauriwa kufanya Kazi na kuziainisha na mpango Kazi wa Serikali wa Miaka mitano, Ili mchango wao uonekane. Kuongeza Usalama katika Ofisi yao. Na pia kutumia ipasavyo Watetezi TV katika kuhabarisha jamii juu ya masuala ya Haki za Binadamu.

Hata hivyo Shirika la SAWAU limeushukuru mtandao kwa kutoa msaada wa kisheria baada ya Mkurugenzi wa shirika Hilo Bi Sophia Donald Kukamatwa na Jeshi la polisi wakati wa utekelezaji wa mradi wa utoaji wa elimu ya Afya ya uzazi kwa vijana ndani na Nje ya shule, ikiwa ni mojawapo ya majukumu yanayofanywa na Mtandao kwa wanachama.

MWISHO