February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA RAFIKI SOCIAL DEVELOPMENT ORGANIZATION (RAFIKI SDO)

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Shirika la Rafiki SDO, ambalo linafanya Kazi katika wilaya Tano za mikoa miwili ya Shinyanga na Mara.

Katika maadhimisho ya 7 ya Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania Shirika la Rafiki SDO lilifanikiwa kutwaa Tuzo Kutokana na kufanya vizuri katika utetezi wa Haki za Binadamu (livelihood and People’s Welfare).

Rafiki SDO inaendesha mradi wa ‘Waache Wasome’ ambao umeanza mwaka 2017 na kuwashirikisha RAFIKI SDO mwaka 2019 huku ukitarajiwa kukamilika mwaka 2021, mradi huu unalenga kumwezesha mtoto wa kike kubaki shuleni, na Kwa walioshindwa kuendelea na shule kupata nafasi ya kupata elimu Nje ya mfumo rasmi wa Elimu Ili kuweza kufikia malengo yake.

Katika mkoa wa Musoma taasisi ya Rafiki SDO inaendesha mradi wa vilabu vya masomo ya Sayansi, hisabati, na kompyuta kwani masomo hayo yanaaminika Kuwa sababu Kuu ya wanafunzi kutomaliza masomo yao, lakini pia walimu na wazazi hujengewa uwezo wa kuweza kutambua viashiria vinavyoomyesha iwapo mwanafunzi ana dalili za kuacha shule lakini pia kuripoti dalili hizo Ili kuweza kumnusuru mwanafunzi.

Mradi huu unaendeshwa katika shule 15 ndani ya kata 16 za mkoa wa Mara ambao umefanikiwa kuwafikia wanafuzi 750 kwa shule 15 zenye wanafunzi 50 kwa kila klabu.

Taasisi imefanikiwa kuwafikia watoto 128 wa Nje ya shule, Shirika limefanikiwa kubaki na wanufaika 254 wa mradi.

Rafiki SDO Inaendesha vikundi 112 vyenye wanachama 30 kwa kila kata ambavyo vimefanikiwa kuwasaidia wanachama kujikwamua kiuchumi katika uendeshaji wa shughuli mbali mbali.

Rafiki SDO inakumbana na changamoto katika uendeshaji wa miradi ya klabu za mashuleni hasa Kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo wa wazazi juu ya masomo ya watoto wanayosoma mashuleni hivyo hushindwa kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada.

Mila na desturi za wakazi wa mkoa wa Mara zinachangia kwa kiasi kikubwa kusua au kwa miradi inayolenga kumwezesha mtoto wa kike kutjitambua, pamoja na uelewa mdogo wa Jamii juu ya umuhimu wa mtoto wa kike katika upataji wa Elimu.

Mratibu THRDC alipata wasaha wa kutembelea kituo cha SIDO Cha mkoa wa Mara na kuzungumza Pamoja na kuutambulisha Mtandao kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho ambapo kikundi cha Ujasiriamali kilichowezeshwa na Taasisi ya Rafiki SDO kimeweza kujifunza Kazi mbali mbali za Ujasiriamali utakaokiwezesha kujitegemea kiuchumi.

Mratibu ameipongeza taasisi ya Rafiki SDO kwa Kazi kubwa inayofanya katika kuisaidia jamii ya mkoa wa Mara na Wilaya zake na kuisihi taasisi kuendelea na kasi hiyo ambayo inanufaisha wakazi wa mkoa huo.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC