February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA MIKONO YETU

Na Loveness Muhagazi

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa akiongozana na Afisa dawati la wanachama Bi Lisa Kagaruki, Pamoja na Mwakilishi wa Mratibu wa Kanda ya Ziwa wametembelea shirika la Mikono Yetu Centre For Creativity and Innovation (Mikono Yetu).

Mikono Yetu linaendesha programu nne mpaka sasa ambazo zimejikita katika masuala ya haki ya mwanamke na msichana. Programu hizi ni,
1) Uwezeshaji wanawake kiuchumi (Women Economic Empowerment), Programu hii inahusisha ujasiriamali kwa upande wa mwanamke, na kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa viwanda vya usindikaji kwa ajili ya kuongeza thamani ya bidhaa zao. Programu hii ina jumla ya vikundi 6 vya wanawake katika eneo la Sengerema.
2) Uwezeshaji Wasichana (Girls Empowerment), Programu hii inafanya kazi kwa bango kubwa la “Msichana ni Tai” iliyoanza mwaka 2019 kwa udhamini wa NOVA Foundation. Programu hii inahusika na kuwajengea uwezo wasichana wenye umri wa miaka 9-20, walioko nje ya shule. Kwa sasa imewafikia wasichana 445 kwa kata ya Buswelu. Kupitia hii programu, msichana hujiona wa thamani katika jamii kwa kuweza kufikia ndoto zao. Kwa mfano, uanzishaji wa “Msichana TV” ambayo ni TV yenye ndoto kubwa sana. Pia wasichana hawa hupewa elimu ya uzazi.
3) Programu za Mazingira kwa wanawake.
4)Programu ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia

Pamoja na Kazi zinazofanywa ana Shirika la Mikono yetu, katika miradi tajwa, Bado Shirika hili linakiri kukumbana ma Changamoto mbalimbali ikiwemo, Janga la UVIKO 19 llililopelekea ufanyaji Kazi kwa kupokezana Ili kupunguza athari za maambukizi ya Janga hili, Upatikanaji wa vibali vya kufanyia kazi kutoka kwa mamlaka husika, jamii hasa walezi wa wasichana kutokuchukua hatua changamoto zinapotokea na kuamini kuwa Kazi za utetezi katika jamii Kuwa za Watetezi pekee, hivyo hata penye uwezekano wa kusaidia wamekuwa wakikaa kimya, changamoto za kifedha katika jamii zinazohusishwa kuchangia kuongeza uvunjwaji wa Haki za kundi hili la wanawake.

Shirika la Mikono yetu linakiri Kuwa na mafanikio kadhaa ambayo yamepatikana katika Shirika kwani Kwa sasa limekuza bajeti yake ya mwaka, kuongeza wafanyakazi walioajiriwa, Shirika limeweza kufungua televisheni ya “Msichana TV” ambayo imekuwa ikirusha vipindi vya Haki za binadamu Pamoja na kutoa elimu katika maeneo mbali mbali ya utetezi, katika hili Shirika la Mikono Yetu limekuwa likiwasaidia mabinti walio katika Mazingira hatarishi Nje ya shule kupata elimu isiyo rasmi katika kuwapatia Mafunzo ya uendeshajibwa vipindi vya televisheni Pamoja na utangazaji, elimu ya urembo kwa wale wanaopwnda masuala ya ususi kwa kuwapeleka katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kujifunza, Shirika pia linaendesha Mafunzo ya Ujasiriamali na katika Hilo limeweza kuanza ujenzi wa kiwand acha usindikaji kitakachowasaidia wanawake kuweza kupata elimu ya usindikaji wa Bidhaa mbali mblai za vyakula iliqemo mmea wa Rozela Lakini pia kupitia mafunzo mbalimbali yanayotolewa na THRDC, Shirika la Mikono Yetu limeweza kuweka camera za usalama (CCTV Cameras) kwa ajili ya kuboresha ulinzi na Usalama wa Shirika.

Mratibu THRDC amehimiza juu ya kuendelea kuweka rekodi nzuri ya changamoto zinazotokana na UVIKO19, Pamoja na na kuendelea kufanya kazir na kuainisha na mpango kazi wa serikali wa miaka mitano, ili kuonesha mchango wa sekta ya AZAKI katika jamii. Taasisi ya Mikono Yetu imeshauriwa pia kutumia ipasavyo televisheni ya Watetezi TV katika kuhabarisha jamii juu ya kazi zao, na hata kuungana na Msichana TV ili kuhabarisha zaidi juu ya masuala ya Haki za binadamu.

Zaidi Kuhusu Msichana TV
Ni channeli iliyoanzishwa na Mikono Yetu kupitia wasichana wenye kipaji cha uandishi wa habari. Hadi sasa, TV hii inatumia cable na inawafikia hadi watu 50,000. Wasichana hao wana maono mbalimbali ikiwemo kuendelezwa kitaaluma katika tasnia he ya habari. Mikono Yetu imeweza kufanya mawasiliano ya awali na SIDO, ITV, HakiElimu na Action Aid juu ya maendeleo ya Msichana TV.

MWISHO