February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA LAKE VICTORIA DISABILITY CENTRE

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Shirika la Lake Victoria Disability centre lililopo walaya ya Butiama mkoani Mara.

Lake Victoria Disability Centre ni Shirika linalojishughulisha na shughuli za utoaji huduma ya Afya, kulisaidia kundi la watu wenye Ulemavu, Pamoja na utoaji wa Mafunzo ya ufundi kwa jamii iliyopo ndani na Nje ya mkoa wa Mara n ahadi Sasa Shirika limeweza kuwanufaisha zaidi yay wanafunzi 3000 ambao wamelifikia Shirika Hilo kwa ajili ya msaada.

Kituo cha lake Victoria ilianza kama Shirika la usaidizi wa watu wenye Ulemavu lakini kadri uhitaji ulivyoongezeka ilifanikiwa kuongeza miundombinu na kufungua kituo cha watu wenye Ulemavu ambacho kumekuwa kikipokea Makundi yote ya watu wenye Ulemavu, na kuwapatia huduma mbali mbali ikiwa ni Pamoja na Mafunzo kwa vitendo (Mafunzo ya ufundi wa vitu mbali mbali), Kuwafanyisha mazoezi baadhi ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo na Kwa ujumla huduma hizo zimekuwa zikilinufaisha kundi kubwa la jamii ya mkoa wa Mara na maeneo jirani.

Taasisi hii iliyoanza mwaka 2002, Ina jumla ya wanafunzi 400, 300 Kati yao wanasoma kwa ufadhili wa Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, hata hivyo taasisi imekuwa ikifanya Kazi na jamii zaidi ambapo watoto wenye Ulemavu wamekuwa wakipata usaidizi katika kituo hicho.

Taasisi ya Lake Victoria Disability centre imekuwa ikifanya Kazi kwa karibu na Serikali ambapo imeweza kuingia katika kamati ya PWD ya wilaya lakini pia hata katika ngazi ya mkoa taasisi imekuwa ikipokea watu wenye uhitaji Baada ya kuagizwa na hospitali Ili kupatiwa usaidizi wa vifaa vya usaidizi kulingana na aina ya Ulemavu Pamoja na kufanyiwa mazoezi.

Taasisi imefanikiwa kufungua karakana tofauti tofauti ambazo zinafanya Kazi ya kutengeneza mabomba, Viti mwendo Pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya kundi la watu wenye Ulemavu, karakana ya ushonaji, Pamoja na eneo la utengenezaji wa viungo bandia kwa ajili ya wahitaji jambo ambalo limekuwa likiwanifaiaha wananchi pmaoja na kundi hili .

Pamoja na mafanikio haya Shirika hili bado linakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo uhaba wa Fedha za kuendeshwa y miradi Pamoja na ambazo zimekuwa Ikisiaaja hasa katika kipindi hiki Cha mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19, mtazamo hasi kwa Jamii juu ya wanafunzi wanaopata elimu katika kituo hiki Cha Lake Victoria kwani jamii imekuwa ikitumia lugha ngumu katika kulitaja kundi la wanafunzi wenye Ulemavu wanaosoma katika shule hiyo, hata familia Bado zinawaficha Watoto majumbani jambo linalopelekea ucheleweshwaji wa upatiwaji wa huduma matibabu hasa kwa kesi za magonjwa yanayotibika.

Changamoto ya kipato inatajwa Kuwa kubwa zaidi kwa familia zenye Watoto wenye Ulemavu hasa ukizingatia mahitaji yao ambayo yanahusisha gharama kubwa ambazo kwa kiasi kikubwa familia zenye Watoto wa kundi Hilo huahindwa kumudu.

Naye Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa ameishauri taasisi kushirikiana na Wadau wengine wa sekta ikiwemo kujiunga katika mitandao mbali mbali Ili kuweza kuwezesha shughuli za Taasisi kutambulika zaidi na kuwezesha wafadhili Kuwa na hamasa ya kuingia kuisaidia taasisi katika ufadhili wa miradi, lakini pia Mratibu ameikabidhi taasisi ya Lake Victoria Disability centre majarida na machpisho yaliyoandaliwa na Mtandao yenye lengo la kuwaelekeza wanachama wa Mtandao namna Bora ya kuendana na sheria na taratibu Ilizowekwa na katika usimamizi wa Mashirika lakini pia kuwawezesha kufanya ‘Compliance’ na kuepuka kadhia mbali mbali katika ufanyaji Kazi za utetezi wa Haki za Binadamu.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC