February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA HOPE FOR GIRLS AND WOMEN

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa Akiwa wilaya ni Serengeti mkoani Mara amefanikiwa kutembelea taasisi ya Hope Girls and Women inayojishughulisha na Kupinga ukatili wa kijinsia (GBV) ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni.

Taasisi ya Hope for Girls imekuwa ikiendesha nyumba salama ambayo imekuwa ikipokea na kuwahifadhi mabinti waliokimbia madhila mbali mbali katika jamii zao na kuwatunza katika nyumba salama huku wenye uwezo wa kurudi mashuleni wakirudishwa na wasio na uwezo kufundishwa stadi za maisha ikiwemo ushonaji, Pamoja na ubunifu, utakaowawezesha kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha, kuwaendeleza kielimu, huku ikivifikia vijiji 87 ambapo kwa kila kijiji huwa mama mmoja aliyepewa Mafunzo na kukabidjiwa simu janja inayomsaidia kuripoti maswala ya ukatili wa kijinsia kupitia App Maalum iliyoanzishwa na Kituo ili kuripoti maswala ya ukatili.

Tangu kuanzishwa kwa kituo mwaka 2017 taasisi imefanikiwa kuwaokoa watoto 1807 waliokimbia ukatili lakini pia taasisi imekuwa ikipokea watoto wadogo ambao wamekuwa wakitelekezwa au kutupwa porini na wazazi wao Baada ya kujifungua.

Mkurugenzi wa Shirika la Hope bi Rhobi Samwel Anaeleza Kuwa katika msimu wa ukeketaji kituo cha hope hupokea mabinti zaidi ya 200 ambao hukimbia ukeketaji na Kuwahifadhi na hii huwa kwa kituo kimoja tu Cha Serengeti ukiacha kituo cha Butiama ambacho nacho kilipokea mabinti wengine 222 Kwa mwaka 2020 hivyo hupelekea kituo Kuwa na kundi kubwa la mabinti wapatao 500 na kuendelea, Hawa ni iwapo watajumuishwa na mabinti zaidi ya 60- 70 waliopo kituoni wanaoshindwa kukubalika kwaa familia zao hasa Baada ya kukimbia pindi walipohitajika kukeketwa au kuozeshwa, kwa mwaka huu taasisi Ina maabinti wapatao 63 ambapo 11 wamefanikiwa kuepelekwa katika shule za bweni huku 53 wakisalia kituoni.

Taasisi imefanikiwa kuwashawishi mangariba kubadilika, kuweka vifaa vya ukeketaji chini na kujiunga katika shughuli za uelimishaji jamii juu ya athari za ukeketaji. taasisi imefanikiwa kumiliki eneo la Hekari 200 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba salama, lakini ilpia imekuwa ikifuatilia mwenendo wa mtoto Baada ya kurudishwa kwa jamii yake.

Taaisisi ya Hope hukumbana na changamoto kadhaa ikiwemo uelewa mdogo wa jamii juu ya athari za ukeketaji na mimba za utotoni, lakini pia uendeshaji wa nyumba salama huwa na changamoto mbali mbali hii ni endapo kituo kitapokea idadi kubwa ya Mabinti kuliko bajeti iliyowekwa jambo ambalo huifanya taasisi kuelemewa na mzigo mkubwa wa kuwalea mambinti ambao hawawezi kurudishwa makwao hasa Baada ya kukimbia changamoto, kumekuwa na changamoto za kifedha, kiusalama hasa kutoka kwa wazazi walionyang’anywa mabinti waliotakiwa kukeketwa, msaada kidogo kutoka kwa viongozi na hasa wanasiasa ambao huungana na jamii na kuwahamasisha kuendelea na Mila hizo Ili kujipatia kura wakati wa kampeni n.k

Mratibu THRDC ameipongeza taasisi ya Hope for Girls kwa kuendelea akufanyaa Kazi kubwa ya kuisaidia jamii, na kuahidi kuendelea kuIpatia taasisi Mafunzo ya Usalama kutoka kwa Mtandao Ili kuiwezesha taasisi kufahamu namna ya kuendana na jamii inayoizunguka hasa katika Utekelezaji wa Kazi za Taasisi bila kupata madhara makubwa, lakini zaidi kuisaidia taasisi kufahamu namna Bora ya kuandika ripoti na kutunza rekodi mbali mbali za shughuli za kitaasisi.

Imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC