Na Loveness Muhagazi
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa katika ziara yake inayoendelea Jijini Mwanza ametembelea shirika la Fadhili Teens Organization.
Shirika la Fadhili Teens linaendesha programu zinazolenga kukuza usawa wa kijinsia, na kuhakikisha upatikanaji wa habari kwa makundi mbalimbali ikiwemo wasiojiweza kiuchumi.

Baadhi ya programu zinazotolewa Shirika hili ni Pamoja na Programu ya Msichana Initiative katika eneo la Sengerema ambapo Programu hii inaahakikisha mabinti wanapata Haki yao ya Elimu na wanafanikiwa kumaliza shule, 2)Uhamasishaji wa kiuchumi kwa wasichana katika eneo la Magu.
3) Uhamasishaji wa ulinzi wa Haki za mtoto hasa watoto wenye ulemavu, Pamoja na kuwasaidia wazazi wenye watoto hao kuinuka kiuchumi na kuweza kuwasaidia watoto wao.
Pamoja na miradi hiyo taasisi ya Fadhili Teens inakiri kukutana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo Changamoto ya kiusalama kwa watendaji na maafisa wa Shirika Hilo wanaotekeleza miraadi hiyo katika maeneo mbali mbali, uchache za Rasilimali fedha, Ushirikiano mdogo kutoka kwa walimu hasa pale Shirika linapotekeleza miradi katika shule mbali mbali.

Hata hivyo taasisi ya Fadhili Teens imekuwa na mashirikiano Mazuri na serikali, jamii, pamoja na mashirika mbalimbali ikiwemo SAWAU, Mikono Yetu, na hata Shirika la Amani Girls ambao wote ni Wanachama wa Mtandao.
“Muhimu ni kuwepo na mshikamano na uratibu mzuri wa Mtandao kwa ngazi ya kanda, na hata kimkoa, Kwani Umoja wa wanachama wa Mtandao wa THRDC ukiimarika, utasaidia kuongeza nguvu katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu kwa mkoa wa Mwanza” Atanas Bagenyi Mkurugenzi wa Shirika la Fadhili Teens
Naye Mratibu THRDC amehimiza Tasisi ya Fadhili kutumia mwongozo wa wanachama Ili kuendana na sheria, lakini pia ameitaka taasisi hiyo kupitia mpango wa Utekelezaji wa AZAKI wa maendeleo ya Taifa wa Miaka mitano kwani shughuli zinazofanywa na Taasisi za Watetezi wa Haki za Binadamu zimetajwa katika mpango huo. Pamoja na hayo Mratibu amehimiza suala la utakelezaji wa sheria “compliance” ili kuepuka adhabu mbalimbali kisheria.
MWISHO
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.