February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU THRDC KATIKA SHIRIKA LA AMANI GIRLS HOME

Na Loveness Muhagazi

Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa hii leo anetembelea Shirika la Amani Girls Home.

Shirika la Amani Girls limekuwa likifanya kazi za utetezi wa haki za watoto wa kike mwenye umri wa kati ya miaka 3 hadi 13 ambao wanakumbwa na madhila mbali mbali na waishio katika mazingira hatarishi nchini Tanzania na nje, Shirika limekuwa likiwachukua mabinti hao na kuwaweka chini ya uangalizi kwa muda usiozidi miezi mitatu huku likitafuta ufumbuzi wa matatizo yao kwa kufaya mazungumzo na familia zao na kwa kesi ambazo zinashindikana Watoto hao hupelekwa katika nyumba salama kwa malezi Zaidi.

Katika kazi hizi shirika la Amani limekuwa likishirikiana na serikali kuputia jeshi la polisi, jamii kwa ujumla, Pamoja na shirika la SOS Childrens Home Villages Tanzania hii ni katika kuhakikisha mtoto wa kike anaishi katika mazingira mazuri na salama.

Pamoja na shughuli za utetezi shirika la Amani Girls limekuwa likiendesha miradi ya utetezi wa haki za wanawake, Watoto Pamoja na vijana ili kuwawezesha kupatiwa haki zao pindi zinapovunjwa, kuvisaidia vikundi vya wanawake kuinuka kiuchumi ili kuwa na uwezo wa kuwalea Watoto wao vizuri, Ukuaji wa elimu ya awali kwa kushirikiana na serkali na wananchi kusimaia masuala ya elimu, nah ii imepelekea kupungua kwa idadi ya kundi la Watoto wa mtaani.

Shirika la Amani Girls linataja mafanikio lililoyapata kwa kipindi cha miaka minne nyuma ambapo kwa mwaka 2020 pekee jumla ya Watoto 115 waliweza kuunganishwa na familia zao, mwaka 2019 watoto 85, Mwaka 2018 watoto 119 na mwaka 2017 watoto 191 ambapo ni idadi kubwa Zaidi kuliko miaka mingine.

Amani Girls imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali katika kutokomeza masuala ya ukatili kwa mabinti kwa kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo kufikia na kuyaeimisha makundi kupitia ngoma za Asili, Kuwatumia viongozi wa dini ambao wamekuwa wakiaminika sana na jamii, kuwatumia vijana wa boda boda vijiweni, n ahata katika vijiwe vya kahawa ambapo shirika limekuwa likitoa vibao vya mchezi wa Drafti, vyenye jumbe za uelimishaji juu ya ulinzi wa haki za mtoto wa kike.

Pamoja na kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa na shirika la Amani Girls bado linakiri kukumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo uelewa mdogo wa jamii juu ya malengo ya shirika katika kumsaidia mtoto wa kike, Kutokuwepo na hamasa ya usaidizi wwa kupambana na maswala ya ukatili wa Watoto wa kike kutoka kwa viongozi wa serikali za mtaa na wenyeviti wa vijiji ambao mara nyingine wamekuwa wakiona vitendo vya ukatili ni kawaida tu, Pamoja na Ucheleweshwaji/ uzungushwaji katika upatikanaji wa vibali katika tafiti.

Hata hivyo Mratibu THRDC ameleezea na kuonyesha kuzitambua changamoto za upatikanaji wa vibali pindi mashirika yanapotaka kufanya Tafiti, na kuahidi kulifuatilia suala hilo kwa kuzungumza na mamlaka husika ili kuangalia mbinu zitakazowezesha utatuzi wa changamoto hiyo kama mtandao ili kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanapata nafasi ya kutekeleza wa miradi kwa wakati, Mratibu ameikabidhi taasisi ya AMANI GIRLS majarida ya Compliance na kusisitiza kuendelea kuzingatia Usalama wao katika ufanyaji Kazi unaozingatia sheria na ameitaka taasisi hiyo kuangalia mpango wa tatu wa maendeleo wa serikaliambao umeainisha shuguli zinazotakiwa kutekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka mitano ili taasi ione ni wapi inapoweza kuingia hii ni katika kuweza kuionyesha serikali kuwa AZAKI ni wadau wakubwa wa maendeleo nchini Tanzania

MWISHO