February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZIARA YA MRATIBU KITAIFA KWA SHIRIKA CENTRE FOR WIDOWS AND CHILDREN ASSISTANCE (CWCA)

Na Loveness Muhagazi

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Onesmo Olengurumwa akiongozana na Afisa dawati la wanachama, Bi Lisa Kagaruki, watembelea shirika la Centre for Widows and Children Assistance (CWCA) tawi la Musoma.

CWCA linahuhusisha na kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wajane Tanzania pamoja na watoto walio kwenye mazingira magumu, pamoja na uhamasishaji wa kiuchumi kwa wasichana. Mratibu wa kanda ya Mara, Bw Nimrod Swai aelezea kwa ufupi historia ya shirika hilo. Dhamira kuu ya CWCA ni kuunda jamii salama inayoheshimu misingi ya kisheria.

CWCA imekua ikitoa elimu na msaada wa kisheria kwa jamii inayowazunguka. Katika kuhakikisha elimu na huduma inafika mbali, CWCA kwa kushirikiana na Legal Service Facility (LSF) imeweza kuratibu vitu 7 vya wasaidizi wa kisheria(paralegals), ambapo kwa ujumla ni wasaidizi zaidi ya 110. Wasaidizi hawa wote wamesajiliwa kisheria. Hii imewawezesha CWCA kufika katika maeneo mengi zaidi kwa mkoa wa Mara.

Shirika hili limepokea changamoto kadhaa pia, ikiwemo changamoto ya kikoo ambapo mkoa wa Mara unasifika kua na koo zenye misimamo sana. Hii imepelekea shirika kupata ugumu kufkisha ujumbe kwa jamii husika. Changamoto za kifedha pia imeikumba shirika hili, hii imepelekea upotevu wa mawakili kwasababu shirika imeshindwa kufkia malipo elekezi ya wakili. Pia shirika hili lilipokea changamoto zilizotokana na janga la UVIKO 19 ikiwemo kukosekana kwa wafadhili.

Mratibu awapongeza shirika la CWCA, na awaelezea kuwa kazi wanayofanya ni kubwa sana. Awahimiza kuendelea kufanya mwendo huohuo, na kuendeleza kasi ya kujulikana na kutambulika kwa jamii na wadau.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania