February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ZAMBIA: TUME YA UCHAGUZI YAMTANGAZA MSHINDI MGOMBEA WA UPINZANI HICHILEMA, AMBWAGA CHINI RAIS EDGAR LUNGU

Na: Anthony Rwekaza

Baada kuingia kwenye kinyanganyiro cha Urais kwa mihula mitano kwa tiketi ya Chama Cha Upinzani cha UPND Hakalinde Hichilema ametangazwa na Tume ya Uchaguzi Nchini Zambia kuibuka mshindi kwenye kiti cha Urais, akimpiku Rais Edgar Lungu alikuwa akitetea kiti chake kwa muhula mwingine.

Akitantangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika alhamisi 12, Augosti 2021, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi ya Zambia Esau Chulu alfajiri ya kuamkia leo Jumatatu 16, Augosti 2021, amemtangaza Hakainde Hichilema wa chama cha United Party for National Development (UPND) kuwa amepata kura 2,810,777 akimpiku Rais wa aliyekuwa akitetea kiti chake Edgar Lungu kwa tiketi ya chama cha Patriotic Front (PF) aliyepata kura 1,814,201.

Taarifa hiyo ilikuwa ni ya jumla ikijumuhisha vituo vyote vya uchaguzi kwenye Majibo 156, na imeelezwa wapiga kura milion 7 na zaidi walijiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo, huku taarifa za awali zilizokuwa zikitolewa na Tume hiyo kwenye vituo tofauti zilimtaja Hichilema kuongoza kwa kula nyingi, lakini katika hali ya kushangaza ni pale mgombea huyo alipoibuka na kula nyingi kwenye kituo kinachozunguka Ikulu ya Zambia kichotajwa kuwa ni sehemu yenye makazi ya maafisa wengi ya waliohudumu kwenye Serikali ya Rais Lungu.

Hakalinde Hichilema ambaye ni Mchumi na mfanyabiashara maarufu Nchini Zambia mwenye umri wa miaka 59, ameshiriki kwenye kinyanganyiro cha Urais mara tano, lakini kwa sasa ametangazwa kuwa Rais Mteule wa Taifa hilo lenye wakazi zaidi ya milioni 19 na kama akiapishwa atakuwa Rais wa nane wa Taifa ilo tokea lilipo pata uhuru chini ya Rais wa kwanza Keneth Kaunda ambaye zimepita wiki chache tokea iripotiwe taarifa ya kufariki kwake.

Aidha kwa upande wa Mgombea wa chama cha PF, Edgar Lungu kwenye kinyanganyiro alikuwa akitetea kiti chake kwenye muhula mwingine baada ya kupokea kiti kutoka kwa mtangulizi wake aliyedumu kwa muda mfupi Rais Guy Scott.

Licha pia ya kuzidiwa kura zaidi milioni moja Rais Rungu wakati taarifa za majumuisho ya jumla ya kura zote haijatolewa kwa umma alidai uchanguzi huo haukuzingatia uhuru na haki kutokana na taarifa za kula alizokuwa anazipata kwenye majimbo mbalimbali hata yale ambayo aliamini ni ngome yake, lakini baada ya masaa machache baada ya Hichilema kutangazwa mshindi ametangaza kukubali matokeo na kumpongeza kwa ushindi huo.

Sababu zinazotajwa kumuangusha mwanasiasa Rais Edgar Lungu ni pamoja na mdololo wa Uchumi kwa wananchi wa Zambia, mfumuko wa bei kwenye bidhaa na huduma muhimu, huku sababu ya changamoto ya ukosefu wa ajira hasa kwa vijana ikitajwa kama mwiba mwingine uliomuagusha.

Matamio ya wananchi wengi yanaonyesha matumaini kwa Rais Mteule Hakalinde Hechilema kuwa kutokana na uzoefu wake kwenye masuala ya Uchumi anaweza kuwa muharobaini wa changamoto hizo zilizochangia kuanguka kwa mshindani wake.

Kufatia hatua za awali za kumtangaza mshindi kukamilika, kwa taratibu za Tume ya uchaguzi Zambia watatoa taratibu zote za kisheria na zikikamilika kwa usahihi watatangaza tarehe maalumu za kumuapisha Rais Mteule Hakalinde Hechilema kuwa Rais mpya wa Zambia kwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi hiyo.

Lakini Rais huyo Mteule, Hakalinde Hechilema baada ya kutangazwa mshindi akizungumza na vyombo vya habari Nchini Zambia amewashukuru wapiga kura kwa kuamua kufanya mabadliko huku akiadi kudumisha uhuru na Demokrasia, kuinua Uchumi wa Taifa hilo na kulinda vyema haki za binadamu.