February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WAZIRI UMMY ATOA MAAGIZO MAZITO, KUFATIA VIFO VITATU SHULE MOJA

Na Antony Benedictor

Kufuatia vifo vya wanafunzi watatu waliofariki kwa kufukiwa na kifusi, Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameagiza walimu wote wa shule ya msingi Mbori iliyoko Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma walipokuwa wakisoma wanafunzi hao kusimamishwa kupisha uchunguzi.

Taarifa zilizoelezwa awali zinasema kuwa Wanafunzi hao waliangukiwa na kifusi wakichota mchanga wa kujengea choo cha shule hiyo jambo limeibua sintofahamu, na kupelekea Waziri Ummy kutoa maamuzi hayo.

Akielekeza maagizo hayo wakati wa kuaga miili ya Wanafunzi hao, pia amesema baada ya uchunguzi kukamilika watakaobainika kufanya uzembe wowote uliopelekea vifo hivyo wachukuliwe hatua kisheria.