February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WAZIRI MKUU APOKEA RIPOTI YA MAPENDEKEZO YA WANANCHI WA NGORONGORO

Wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa kuratibu mapendekezo ya wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi unaoendelea katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro,Emmanuel Shangai hapo jana jijini Dodoma wamekutana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na kumkabidhi ripoti ya mapendekezo hayo.

Kamati hiyo yenye wajumbe 60 inawajumuisha wawakilishi waMadiwani,wenyeviti,wanawake, viongozi wa kimila na baadhi ya wasomi wa jamii hiyo ya kifugaji na ilianza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi katika vijjji vyote vinavyozunguka eneo lenye mgogoro wa kilomita za mraba 1500 pamoja na vijjji vyote vya Tarafa ya Ngorongoro.

Akipokea Ripoti ya Mapendekezo hayo, Waziri Mkuu amesema mipango ya serikali kamwe  haiwezi kuwa na nia mbaya kwa watu wake na kueleza serikali inapanga kuanza kutoa elimu juu ya namna bora ya ufugaji.

“Taarifa nimezipokea zote mbili,zinazozungumza,zinazoshauri namna nzuri ya kuhifadhi lakini pia inawezekana mmeandika namna nzuri ya kutekeleza zoezi hili,”amesema Majaliwa akiongeza kuwa serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili walioamua kufuga wilayani humo wapate tija.

“miaka mingi tumeacha watu wanachunga sio kufuga ,nataka sasa tuanze kuelimisha namna bora ya kufuga mifugo hii serikali inatupatia mapato lakini watanzania wanaoshughulika na mifugo inawapatia mapato,”amesema Majaliwa.