February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WAZIRI MKUU ABAINI UPIGAJI MSD, AELEZA MADUDU YA KUTISHA

Na: Anthony Rwekaza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amkute katika ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) Jumatatu Mei 9, 2022 saa nne asubuhi, ikiwa baada ya kubaini ubadhirifu wa fedha za Umma katika ununuzi wa vifaa vya matibabu kinyume na uhalisia wa soko.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo katika ufunguzi wa Wiki ya Ununuzi wa Umma jijini Arusha Mei 5, 2022, ambapo amesema kuwa gharama kubwa imeonekana kutumiwa na MSD kununua vifaa tofauti na bei halisi za soko, ambapo amedai kuwa hali hiyo imepelekea Serika kupoteza fedha nyingi za na kusababisha Wananchi huduma stahiki kwani vifaa kutokana na kushindwa kununua vifaa vinavyojitosheleza kama ilivyotakiwa.

“Gharama kubwa imetumika kununua vifaa vya matibabu na Bohari ya Dawa (MSD) tofauti na bei halisi za soko, hivyo kupoteza fedha nyingi za umma na kuwakosesha wananchi huduma kwani vifaa vilivyonunuliwa ni vichache” amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Aidha Majaliwa kufuatia kubaini hali hiyo wakati akizungumza na wataalamu wa ununuzi na ugavi, ametaja baadhi ya manunuzi ambayo ya harufu ya ubadhirifu wa fedha za Umma, ambapo maeneo aliyoyataja ni pamoja ununuzi wa kipimo cha haimolojia ambacho bei yake ya soko aliyoitaja ni milioni 37 lakini katika manunuzi ameweka wazi kuwa MSD wameonesha kukinunua Milioni 147.9.

Kipimo kikubwa cha haiemolojia ya mwili ambacho ni shilingi milioni 37, lakini Bohari ya Dawa (MSD) wamenunua kwa shilingi milioni 147.9,” amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,

Katika hali ya kuonesha ubadhirifu huo ambao unadaiwa kufanywa na MSD, Waziri Mkuu amesema kuwa walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000.

“Bohari ya Dawa (MSD) walitakiwa kununua mashine ndogo ya kipimo cha haemolojia ya mwili kwa shilingu milioni 5, lakini wakanunua kwa shilingi milioni 14,045,000” amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Pia Waziri Mkuu ameongez kuwa eneo jingine ambalo linaonesha ubadhirifu ni kipimo kikubwa cha kuchakata maji kwa ajili ya kudafisha damu, ambacho kilitakiwa kununuliwa shilingi milioni 37 kulingana na bei ya soko, lakini MSD amesema kuwa inaonesha kuwa kipimo kilinunuliwa shilingi milioni 147.9, pia walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho kinauzwa milioni 32 lakini wamekinunua kwa shilingi milioni 129.

“Pia Bohari ya Dawa (MSD) walitakiwa kununua mashine ya kuchakata maji kwa ajili ya kusafisha damu ambacho inauzwa shilingi milioni 32 lakini wameinunua kwa shilingi milioni 129” amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatosita kuwachukulia hatua za kinidhamu, amesema kupitia vyombo vya dola wanaweza kuwaweka kando nje ya utumishi ili kupisha hatua nyingine.

“Na mimi sitasita kwenda na Kamanda Sirro, na Kamanda Hamduni, ili washughulike na watu. Lazima tuanze na watu hawa wanaofanya kazi hii, wakae nje, hatua nyingine zifuate,” amesisitiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa