February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WAZIRI DKT. GWAJIMA ASEMA MIKUTANO KIMATAIFA ALIYOSHIRIKI IMEGUSIA HAKI ZA WANAWAKE

Na: Anthony Rwekaza

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt.Dorothy Gwajima ametoa mrejesho wa mikutano miwili ya Kimataifa aliyoshiriki ikiwemo Mkutano wa 66 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali za Wanawake Duniani na Mkutano wa G7 Care Work. Ameota mrejesho huo kwa wadau Jijini Dodoma

Akizungumza na wadau mbalimbali Jijini Dodoma leo Mei 5, 2022, amesema ameitisha kikao ili kutoa mrejesho wa mikutano hiyo na kuweka mikakati ya utekelezaji wa maazimio ya mikutano hiyo ili kujipanga kuw na ushiriki bora zaidi katika mikutano hiyo kwa wakati mwingine.

Waziri huyo amesema kuwa alishiriki mikutano hiyo muhimu kutokana na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kulinda Haki na Usawa wa Kiuchumi kwenye Jukwaa la Usawa wa Kijinsia.

“Nilishiriki katika mikutano hii ni muhimu sana kama mnavyofahamu Mh. Rais Suluhu Samia aliahidi kuwa kinara wa utekelezaji kuhusu Haki na Usawa wa Kiuchumi kwenye Jukwaa la usawa wa Jinsia” Waziri Dkt. Dorothy Gwajima

Pia Dkt Dorothy Gwajima lengo la kushiriki mikutano hiyo ilikuwa ni kwenda kujifunza na kueleza juu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuwezesha wanawake kupata Haki za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Haki za usawa kijisia kiujumla.

Tanzania ikishiriki mikutano hiyo kwa lengo la kwenda kujifunza na kueleza Duniani nini Tanzania inafanya katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na Usawa wa Kijinsia” Waziri Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt. Dorothy Gwajima

Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa lengo la Mikutano hiyo muhimu ilikuwa ikijadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake ikiwa ni pamoja na mafanikio na changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuzipatia uamuzi ya kisera na kiutekelezaji kutoka kwa viongozi na wataalam.

Itakumbukwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa mara kadhaa tokea aingie madarakani amekuwa akisisitiza usawa wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na wanawake kupata fursa sawa za kiuchumi ili kuwezesha Taifa kipiga hatua za maendeleo.