March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WATUMISHI WAWEKWA MGUU SAWA MABADILIKO YA MAHAKAMA MTANDAO

VIONGOZI na watumishi wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuwa tayari kuendana na mabadiliko ya mfumo wake, kutoka mfumo wa analojia kwenda wa kidigitali.
Agizo hilo limetolewa leo Jumanne, jijini Dodoma, katika mkutano wa tatu wa Baraza Kuu la Saba la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.
“Uongozi wa mahakama katika kanda, divisheni na makao makuu kupima utayari wa kila mtumishi kuhama. Pia, kupanga mambo ya kufanya wakati wa mpito kutoka mahakama ya kawaida hadi mahakama ya mtandao ambayo ni endelevu,” amesema Prof. Juma.
Prof. Juma ameagiza uongozi wa mahakama kuzingatia utunzaji wa nyaraka za mahakama katika mchakato wa mabadiliko hayo.
“TEHAMA ina lengo la kuboresha kutufanya tuwe wawazi na kutoa huduma bora. Katika kuhamia mahakama mtandao usalama wa nyaraka za kimahakama na za utoaji haki ni mambo ambayo yatahitaji kujitayarisha kwa kina. Wakati wa mpito ni wakati wa kutathimini usalama wa nyaraka za mahakama,” amesema Prof. Juma.