February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WATU 71,115 WARIPOTI UKATILI KIJINSIA NJE YA MUDA, WAZIRI ATOA NENO

Watu 71,115 kati ya 97,479, walitoa taarifa za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya nje ya muda kisheria.
Hayo yamebainishwa leo Jumatatu, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.
Waziri Ummy amesema, kuanzia Julai 2021 hadi Machi 2022, takribani watu 97,479 walitoa taarifa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kati yao 26,364 walitoa taarifa ndani ya muda sahihi wa masaa 72 tangu kutendewa vitendo hivyo, ikiwa ni sawa na asilimia 27.
“Nitoe wito kwa wahanga wa ukatili kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya ndani ya saa 72 baada ya tukio. Aidha, ninawataka watoa huduma za afya kutowanyanyapaa wahanga wa vitendo hivyo bali wawapatie huduma haraka kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyowekwa,” amesema Waziri Ummy.