February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU (THRDC) WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZ NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA LEO

Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu Tanzania THRDC hii leo umekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi katika ofisi za Wizara hiyo, Mtumba Jijini Dodoma.

Mkutano huo Umelenga kukuza mashirikiano na uhusiano mwema Kati ya Wizara hiyo na Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania Pamoja na kujadili changamoto za kisheria na kiutendaji zinazowakabili Watetezi Pamoja na kuiomba Wizara kuchukua hatua stahiki dhidi ya changamoto hizo.

Miongoni mwa masuala mengi yaliyoibuliwa na Watetezi wa Haki za Binadamu Kati yao ni Pamoja na kuwepo kwa Ushirikiano zaidi Kati ya Wizara na Watetezi wa Haki za Binadamu, Serikali kuruhusu raia wa Tanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kufikia Mahakama ya Afrika, Serikali kuridhia mkataba wa Afrika wa haki za Binadamu na watu hasa kwa kundi la watu wenye ulemavu barani Afrika, uboreshaji wa mifumo ya upatikanaji haki, ikiwemo Maboresho ya sheria mbali mbali, Maboresho ya mfumo wa Haki jinai, Ushiriki wa serikali katika mchakato w akimataifa wa mapitio ya Haki za Binadamu (UPR) na mifumo mwingine ya haki za binadamu huku mtandao ukiiomba Serikali irekebishwe vifungu vya BREDEA Pamoja na kuunda chombo maalumu kwa Ujsimamizi wa polisi Ili kukuza uwajibikaji.

Katika Mkutano Huo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania uliweza kuelezea shughuli zinazofanywa na mtandao huo Pamoja na Wanachama wake zaidi ya 200 walioenea nchini Tanzania Bara na Visiwani.

Mtandao umefanikiwa kuelezea Ushirikiano uliopo Kati ya Wizara hiyo na Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini katika maswala mbali mbali ikiwa ni Pamoja na kuhimiza mabadiliko ya sheria na Sera muhimu pamoja na kuwajengea uwezo baadhi ya watumishi wa Mahakama katika masuala mbali mbali ya Haki za Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania huku wakihamasisha kuwepo kwa uwiano baina ya viwango vya kimataifa vya haki za Binadamu na vya kitaifa.

Wanachama wa THRDC waliojitokeza katika Mkutano huo ni Pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya LHRC, WOWAP, TAWLA, HAKI ELIMU, ZAFAYCO, WOTE SAWA, DOOR OF HOPE, MSICHANA INITIATIVE, NA WAWAKILISHI KUTOKA THRDC.

Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria walipata nafasi ya kushiriki kikao hiyo ni pamoja na Naibu Waziri wa Katiba na sheria Geofrey Pinda, Katibu mkuu Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu mkuu Dkt Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Sarakikya Nkasori, Mkurugenzi wa masuala ya sheria wa Wizara, Pamoja na msajili wa Paralegal.