February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WASIRA ATAKA WENYE NIA YA KUWANIA URAIS 2025 KUBADILI MTAZAMO

Kada wa CCM ambaye aliywai kuwa Mbunge na Waziri kwenye Serikali za awamu zilizopita Steven Wasira, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, huku akiwashauri wanaojipanga kuwania nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM 2025 kwa kuwa utamaduni wa chama icho unatoa nafasi ya kumalizia awamu ya pili.

“Na wale wanaosema wanautaka Urais mwaka 2025 Mimi nawashauri wasubiri kwasababu kwa utamaduni wa CCM kama una Rais aliyopo Ofisini huwa hatumpingi tunampa nafasi amalize kipindi cha awamu hiyo ambayo huchukua miaka 10” amesema Steven Wasira

Pia Wasira amesema kwa wenye nia hiyo ya kutaka kuwania Urais kama wanahisi umri wao utakuwa umeenda mara baada ya Rais Samia kumaliza vipindi vyake viwili, amewashauri waachane na mtazamo huo kama yeye alivyouacha baada ya kuona umri wake umeenda na kuona hawezi kuwania the Urais.

“Kama una umri mkubwa na unafikiri ikipita miaka tisa utazeeka basi acha kwasababu hatuwezi kuwa Marais wote, Mimi niliutaka Urais sasa hivi siutaki tena kwasababu umeshanipita sasa wanakuja wengine, sasa kama na wewe una miaka mingi na una mashaka kama usipoupata mwaka 2025 utachelewa ni bahati mbaya” amesema Steven Wasira

Itakumbukuwa Rais Samia Suluh Hassan kwa wakati tofauti amekuwa akieleza juu ya uwepo wa wanachama wenye nia ya kuwania Urais mwaka 2025, lakini amekuwa akiwataka waelekeze nguvu katika kuwaletea wananchi maendeleo.