February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WASANII, WANAHABARI, WANAMICHEZO KUPATIWA CHANJO DAR

Dkt.Hassan Abbas-Katibu Mkuu,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo.

Na John Mapepele

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeratibu zoezi la hiari kwa wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi, ameeleza kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya  kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Shime kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika,” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz  ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.

Ametoa wito kwa Wasanii, Wanahabari na Wachezaji kwa hiari yao kujitokeza na kutumia fursa  hii kipata chanjo ili kujikinga na kuwakinga wengine na ugonjwa wa UVIKO 19.