December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WANAFUNZI NIGERIA WATEKWA

Watu wenye silaha wamewateka wanafunzi katika shule moja ya Kiislam jimbo la Niger, nchini Nigeria.Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo hilo,Wasiu Abiodun amesema watekaji hao waliwasili katika shule hiyo iliyo kwenye mji wa Tegina wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kufyatua risasi hewani kabla ya kutekeleza utekaji huo.

Ripoti za awali  zinadai kuwa jumla ya  watoto 200 ndio waliokuwa shuleni hapo, na haijafahamika ni watoto wangapi walitekwa na ni wapi walikopelekewa.Hata hivyo,mmoja wa  shule hiyo amesema watoto waliotekwa ni zaidi ya 100 lakini waliokuwa wenye umri kati ya miaka minne na 12 wakarudishwa shuleni.