February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WANACHI HIFADHI YA NGORONGORO HUENDA WAKAKUMBWA NA JANGA LA KIBINADAMU

WANANCHI WA HIFADHI YA NGORONGORO WALIA KUWEKEWA VIKWAZO VYA HUDUMA ZA MSINGI

Baada ya kuzungumza na baadhi ya ndugu zangu na viongozi kule Tarafa ya Ngorongoro nimekutana na taarifa za kusikitisha sana.

Wananchi wanaoishi katika Hifadhi ya Ngorongoro Tarafa ya Ngorongoro wamejikuta katika wimbi kubwa la kutaka kuelekea katika janga la kibadamu baada ya serikali kupitia NCAA Kuweka na kutekeleza mikakati ya kuwazuilia huduma za msingi kwa miaka zaidi ya 7 kuanzia 2016.

Tarafa ya Ngorongoro ni moja ya Tarafa tatu za wilaya ya Ngorongoro inayochukua zaidi ya asilimia 60 ya eneo la wilaya ya Ngorongoro inayokadiriwa kuwa na wakaazi takriban 90 elfu.

Mabadiliko ya sheria ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika 1975 iliweka UDHIBITI mkubwa wa shughuli za binadamu ikiwemo kuzuia kilimo, kutenga maeneo muhimu ya malisho na maji kwa ajili ya wanyama pori pekee, kuchukua maeneo yenye vyanzo vya maji na kuwapa wawekezaji wa biashara ya utalii, kuthibiti makazi na hata matembezi ya watu.

Pamoja na athari hasi zilizotokea na kuwa na sheria inayopendelea uhifadhi na biashara ya utalii hali imekuwa mbaya maradufu mwaka jana na mwaka huu mwanzoni mara baada ya serikali kutangaza nia ya kuwaondoa wafugaji hifadhini.

Wanachofanyiwa wamasai waishio katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ni linaweza leta janga kubwa la kibinadamu. Wananchi wa Ngorongoro wanalia na mpaka sasa hawajasikilizwa na sina uhakika kama vilio hivi vinamfikia Rais Samia.

Hawa watanzania wamelinda rasilimali asili eneo lile kwa zaidi ya maiaka 2000 lakini leo wanachovuna ni kutengwa na kubezwa kila kukicha kutokana na mfumo wao wa Maisha wa Kifugaji wa asili ambao ni rafiki na wanyama pori na mazingira.

Miradi ambayo serikali imezuia kuidhinisha kwa ajili ya maendeleo ya Wamasai hao ni pamoja na kutotoa vibali vya utekelezaji wa miradi ambazo zimepewa fedha na Serikali Kuu, fedha za UVIKO-19, Halmashauri ya Wilaya, Wafadhili na taasisi za dini.

Ifuatayo ni miradi iliyokwama kutekelezwa kwa kukosa vibali toka NCAA;

(a) Miradi ya Afya
1. Kituo cha Afya Nainokanoka Tsh, 500,000,000 Mradi toka TAMISEMI

2. Kituo cha Afya nainokanoka 80,000,000- Mradi wa NCAA.

3. Zahanati ya masamburai, 75,000,000

4. Zahanati ya Ngoile 50,000,000

5. Kituo cha Afya osinoni 115,000,000

(b) Miradi ya maji
1. Mradi wa maji Lemuta -ukarabati wa pampu la majibunaotumia nishati ya upepo wa Tshs 80,000,000

2. Mradi wa maji Alaililai 200,000,000

3. Mradi wa maji Ngoile 200,000,000

4. Mradi wa maji masamburai 151,000,000

(C) Miradi ya Elimu
1. Shule ya sekondari Embarway 100,000,000

2. Shule ya sekondari Nainokanoka 80,000,000

3. Shule ya wasichana Ngorongoro 180,000,000

4. Shule ya msingi Endulen 100,000,000

5. Ereko shule ya msingi 70,000,000

6. Irkipori shule ya msingi 40,000,000

7. Shule ya Msingi Irkeekpusi Shs 40,000,000

8. Shule ya msingi 40,000,000

9. Shule ya msingi Kakesio Shs 20,000,000

10. St Luke Pre&Primary school wamezuia ujenzi wa mabweni, madarasa na jengo la utawala.

Taarifa hizi ni kwa uchache tu, Wamasai wa Ngorongoro wametengwa na makundi mengi ya kijaamii zikiwemo Asasi za Kiraia kwakuwa zinazojitahidi kufanya utetezi kwa ajili yao ni chache sana na nyingi ni zile za kifugaji pekee ambazo zinafanya kazi hii katika mazingira iliyojaa vitisho vingi sana.

Wametengwa pia na vyombo vya Habari, kwa sasa waandishi wengi wako katika maelekezo ya kutoripoti shida na vilio vya Wamasai wa Hifadhi ya Ngorongoro. Pia inashangaza kuwa hata vyombo vikubwa vya nje navyo vimewatupa wananchi.

Makundi mengine ni Bunge la Tanzania ambalo BAADHI ya wabunge wametoa Rai waondolewe kwa Nguvu na hata kuwakashfu. Badhi ya vyombo vichache vya habari pia zimetumika na kusambaza propoganda za kuhamasisha chuki, ukabila, shuhuda zisizo kweli na kufanya uchochezi dhidi ya Wamasai na serikali.

Aidha matamko ya viongozi wa Ngazi za juu serikalini nazo zimezua taharuki kubwa na wasiwasi. Mfano ni tamko la aliyekuwa waziri wa Mali Asili na Utalii aliyesema “Wamasai wa Ngorongoro Asili yao ni Sudan” ,Na hata sasa wakati utambuzi wa makazi ukiendelea wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro hawana uhakika na zoezi hili kama litawafakia.

Wito wangu kwa Serikali,
Tunashauri wakati michakato mingine ya kuhamisha watu waliojitokeza kuhama kwa hiari ikiendelea , tunaomba Waziri Pindi Chana wa Wizara ya Maliasili, agiza wanachi waendelee kupewa huduma za msingi na haki zao za binadamu ziheshimiwe .

Wananchi waendelee kuhudumiwa kama watanzania wengine , michakato ya kuhamisha watu isiwe sababu ya kusitisha huduma za jamii wakati wananchi bado wapo na wanaishi Ngorongoro kwa mujibu wa sheria .

Mh.Waziri Pindi Chana tunaamini utachukua hatua stahiki ili kuona kwamba miradi ya jamii iliyozuiliwa kwq muda mrefu inafunguliwa wakati mazungumnzo na wananchi juu ya kupunguza idadi ya watu ikiendelea.

Nashauri kukwamisha miradi ya maendeleo isitumike kama sababu ya kuwafanya watu wahame kwa kukata tamaa Bali kuhama kweli kuwe kwa hiari. Vinginevyo kutumia mateso kuwalazimisha watu koundoka ni kuwafanya waondoke ili kuokoa amaisha yao.

MAKALA HII NI MAONI BINAFSI YA MWANDISHI KUHUSU MTAZAMO WAKE BINAFSI JUU YA MGOGORO WA NGORONGORO