Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanakutana siku ya Jumatano katika kikao cha 18 kitakachofanyika kwa njia ya mtandao,Kikao hicho kitaongozwa na Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa sasa na watajadili masuala mbalimbali kuhusu EAC.
Pia marais hao watajadiliana kuhusu kuingizwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kama mwanachama mpya wa Jumuiya hiyo, lakini pia kubadilisha kanuni ya akidi wakati viongozi hao wanapokutana kujadili masuala yanayuhusu EAC.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dr. Peter Mathuki amesema kuingia kwa DRC yenye watu karibu Milioni 90 kwenye Jumuiya hiyo, kutasaidia kupanua soko na fursa za kufanya biashara miongoni mwa nchi wanachama.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS