February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WAKILI MADELEKA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Wakili Pater Madeleka amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la Kuchapisha taarifa ya uongo kinyume cha sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Katika hati ya mashitaka imeanisha kuwa Wakili Madeleka alichapisha ujumbe kwenye Mtandao wa Twitter uliosomeka “Huyu ndiye ERENEUS MWESIGWA Ofisa uhamiaji anayeratibu njama za kuniua kwenye Group la Whatsapp pamoja na maofisa uhamiaji wenzake,”

Katika hati hiyo ya mashitaka imesema Wakili Peter Madeleka alichapisha ujumbe huo akijua kuwa sio wa kweli na wenye lengo la kupotosha umma.

Madeleka amefikishwa mahamani hii leo Mei 5,2022 na kusomewa shitaka hilo na Wakili wa serikali Mwandamizi, Esther Martin mbele ya Hakimu Mkazi, Rhoda Ngamilanga.

Wakili Madeleka alikamatwa na Polisi mnamo April 20,2022 na kushikiliwa kituoni kwa takribani siku tano tangu alipokamatwa katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Mawakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  walifungua kesi ya kuomba dhamana namba 16 ya mwaka 2022 mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka,Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ,Mkuu wa Jeshi la Polisi na Afisa wa Makosa ya Jinai Kanda ya Dar es salaam, shauri ambalo lilipangwa kusikilizwa siku ya Jumatatu tarehe 25 Aprili,2022.

Hata hivyo kabla ya shauri hilo kuanza kutajwa mahakamani hapo Wakili Madeleka aliachiwa kwa dhamana ya Polisi