Wakili Peter Madeleka, ameiomba Mahakama kuu, imlazimishe mkurugenzi wa mashitaka ( DPP) kurudisha fedha kiasi cha shilingi milioni 2 alizochukua kutoka kwa wakili huyo anaedai alilazimishwa na DPP kulipa, ili afutiwe mashtaka ya uhujumu uchumi kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo namba 80 ya mwaka 2021,wakili Madeleka anadai hakutendewa haki,baada ya kulazimishwa kukiri kosa,na kisha kurejesha kiasi cha shilingi milioni mbili,kabla ya hukumu ya kesi yake namba 40/2020,ambapo Mahakama ya hakimu mkazi Arusha ilimuamuru kulipa shilingi 200,000 kama faini na kisha kuifuta kesi hiyo.
Adhabu hiyo ndogo ya mahakama kwa Madeleka,inadaiwa kuwa ilikuwa imelainishwa na malipo ya shilingi milioni mbili,katika ofisi ya DPP,na hivyo maamuzi ya mahakama yalikuwa ni kukamilisha mchakato wa mahakama kabla ya kumfutia kesi.
Kesi hiyo imetajwa kwa mara ya kwanza leo Novemba 10,katika Mahakama Kuu, Masijala ya Arusha.
WAKILI ALIYELAZIMISHWA KUKIRI UHUJUMU UCHUMI AOMBA HELA ZAKE.

Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA