February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WABUNGE BUNGE LA AFRIKA WATWANGANA NGUMI

Mwenyekiti wa tume ya Muungano Umoja wa Afrika,Moussa Faki Mahamat amewataka wabunge wa bunge la Afrika kwa watulivu baada ya kuibuka kwa ghasia katika kikao cha bunge la AU Jumatatu huku akieleza ghasia hizo zinachafua taswira ya taasisi hiyo yenye kuheshimiwa.

Ghasia hizo zilizuka wakati wa vikao vilivyokuwa vimepangwa kwa ajili ya kumchagua kiongozi wa Muungano wa Afrika. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vikao hivyo vilivyofanyika vimeripoti kuwa wabunge hao walivutana mashati na kupigana ngumi wakati wa vurugu hizo.