February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

WABUNGE ASKOFU GWAJIMA, JERRY SLAA WAPIGWA ‘STOP’ BUNGENI MIKUTANO MIWILI, KAMATI YAWAKUTA NA HATIA

Na: Anthony Rwekaza

Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa taarifa Bungeni Dodoma kuhusu shauri la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima na Mbunge wa Ukonga Jelly Slaa baada ya kumaliza kuwahoji kwa tuhuma za kuzungumza uongo na kulishushia Bunge hadhi.

Akitoa taarifa hiyo kwenye vikao vya Bunge vilivyoanza leo Jumanne 2021, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema Mbunge Askofu Josephat Gwajima alikiri kauli zote ni zake 100% na kudai kuwa kauli hizo ilikuwa sehemu ya mahubiri hivyo hayakutakiwa kushukiwa kwa namna yoyote, lakini Mwakasaka amedai kamati ilijiridhisha.

“Kamati ilijiridhisha kuwa mahubiri yanayotolewa yanapaswa kuzingatia Sheria za Nchi hivyo kauli zinazotolewa haziwezi kuwa na kinga ya kuhojiwa”amesema, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka

Pia Mwakasaka amesema Askofu Gwajima ni Mbunge na kiongozi hivyo anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii, amedai kuwa atakiwi kuichonganisha mihimili kama ilivyo kwenye kauli zake alizozitoa mpaka kupelekea kuhojiwa mbele ya kamati, huku akiongeza kuwa Gawajima alishindwa kuthibitisha kauli zake mbele ya Kamati kwa kukosa vidhibitisho vya kuwezwesha ushaidi wa kauli zake.

“Gwajima ni Mbunge na Kiongozi kwa hiyo anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, tuhuma za kuchonganisha Mhimili wa Bunge na Serikali au Serikali na Wananchi zinajidhihirisha wazi kwenye kauli za Askofu Gwajima…,Gwajima alishindwa kuthibitisha kauli zake na hana kielelezo chochote kama alivyowaaminisha Wananchi, suala la Viongozi kupewa rushwa hakutoa ushahidi wowote, kamati imemtia hatiani Askofu Gwajima”amesema, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka

Kufuatia hatua ambayo imetafsiriwa na kamati kuwa ni utovu wa nidhamu kwa Mbunge Askofu Gwajima imependekezwa kutoudhuria mikutano ya Bunge miwili au isiyopugua mitatu mfululizo, aidha kamati hiyo imeeleza kuwa Mbunge huyo hakuonyesha kujutia makosa yake, hivyo Bunge limeadhimia Mbunge huyo kutoudhuria mikutano miwili mfululizo.

“Kuhusu adhabu ya utovu wa nidhamu uliokithiri wa Askofu Gwajima ni kuwa kanuni zinataka asihudhurie mfululizo mikutano miwili au isiyopungua mitatu, Kamati ilishangazwa na vitendo alivyovifanya mbele yake na iliona ni dharau…,Askofu Gwajima hakukiri wala kujutia makosa yake, alionyesha dharau hivyo Kamati imemtia hatiani, Bunge linaazimia kuwa apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitisha azimio hili” amesema, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka

Aidha kwa upande wa Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa baada ya kuhojiwa Kamati hiyo imemkuta na hatia ya kusema uongo kwamba mishahara ya Wabunge haikatwi kodi, Mwakasaka ameeleza kuwa Mbunge huyo akiwa mbele ya kamati hakukiri Wala kujutia makosa yake, hivyo Bunge limeazimia asihudhurie mikutano miwili mfululizo na kutoa mapendekezo ya kuondolewa kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP).

“Azimio la Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuhusu hatua za kuchukua kwa Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa kusema uongo kwamba mishahara ya Wabunge haikatwi Kodi, akiwa mbele ya Kamati hakukiri wala kujutia makosa yake hivyo kamati imemtia hatiani hivyo Bunge linaazimia Silaa asihudhurie mikutano miwili mfululizo na aondolewe kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP)” amesema, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka

Ikumbukwe Agosti 21 Spika Job Ndugai aliamuru wabunge wawili, Josephat Gwajima na Jerry Silaa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Mbunge Josephat Gwajima alianza kuhojiwa Agosti 23, 2021 akidaiwa kutoa kauli za upotoshaji kuhusiana na mchakato wa chanjo ya Corona ambayo ameonyesha msimamo wa kutokubaliana nayo, huku Mbunge Jerry Silaa alianza kufika mbele ya kamati hiyo Agosti 24, 2021 kwa tuhuma za madai aliyodaiwa kuyatoa kuwa mishahara ya wabunge haikatwi kodi.