Na Antony Benedicto
Vyama vya NCCR- Mageuzi na ACT- Wazalendo kwa pamoja vimeeleza kusikitishwa kukamatwa na kuendelea kushikiliwa kwa siku mbili kwa viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Vyama hivyo vimetoa wito kwa Polisi kuwaachia viongozi na wanachama hao bila masharti na kisha wametaka viongozi wa Serikali na viongozi wa vyama vya siasa wakae mezani wakutane.
“Tunatoa wito kwa Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Vyama vya siasa nchini tukae chini tuzungumze namna njema ya kufanya siasa bila uhasama, ni wakati sasa wa Viongozi kuzungumza (political dialogue)” imeeleza taarifa hiyo
Taarifa ya pamoja imetolewa na vyama hivyo na kusainiwa na Viongozi wake wakuu Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.
Habari Zaidi
KIKOSI KAZI KITASAIDIA KULETA MARIDHIANO – JK
NI MIAKA MITANO SASA TOKEA LISSU ASHAMBULIWE
SHAHIDI JAMHURI AELEZA KINA MBOWE WALIVYOSUKA MPANGO WA KUTENDA UGAIDI