February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

VITUO VYA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI VYAPEWA SIKU 30 KUJISAJILI

Serikali kupitia Wizara ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum imetoa siku 30 kuanzia trehe 18 Januari mwaka huu kwa makao ya watoto walio katika mazingira hatarishi yasiyo na leseni kuwasilisha maombi ya usajili katika halmashauri husika na kuhakikisha wanakidhi vigezo na kukamilisha taratibu za usajili ndani ya muda uliotolewa.

Aidha serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanikisha zoezi la ukaguzi wa makao ambayo hayajasajiliwa na yaliyokidhi vigezo na masharti ya utoaji wa huduma ili yaombewe usajili ndani ya muda uliotolewa.

Pia imetoa wito kwa wananchi,Maafisa ustawi ,watendaji wa kata na mitaa kutoa ushirikiano katika kutambua makao yasiyosajiliwa na kutoruhusu makao yasiyo na leseni kuanzishwa katika maeneo yao.

Aidha serikali imesema inatambua jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau wanaolea walio katika mzaingira hatarishi katika makao ambayo yanafuata sheria za nchi,taratibu na kanuni za ulinzi na usalama wa watoto wawapo vituoni humo.