February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

VISASI:CHANZO CHA ONGEZEKO LA KESI ZA UBAKAJI ZANZIBAR,NYINGI ZADAIWA NI ZA KUBAMBIKIWA.

Mmoja ya Mawakili wa Zanzibar,Hassan Kijogoo.

Wengi wanasota rumande kukomolewa.

Adhabu pia yatajwa kuwa katili.

Na Leonard Mapuli.

Baadhi ya Mawakili walioshiriki katika mafunzo ya Mawakili wanaoshughulikia kesi zenye maslahi kwa Umma wamesema ongezeko la kesi za uzalilishaji kwa wanawake na watoto visiwani Zanzibar,unatokana na chuki baina ya watu ambapo kesi nyingi watuhumiwa hubambikwa kama kisasi toka watu walionao ugomvi.

Katika mafunzo hayo ya siku mbili chini ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania,Mawakili hao wameahidi kutengeneza umoja utakaolenga kuwasadia watu wanaopewa kesi za uongo kulipiza kisasi.

“Wanaume wengi wanabambikiwa kesi,siyo kwamba watoto wanabakwa,wengine wanaanza kushiriki ngono wakiwa chini ya umri wa miaka 16 ambapo Mahakama inawaweka kundi la Watoto,kwa hiyo ukigombana na mzazi mwenzio ama mtu mwingine anatafuta mtoto wa kike ambae tayari ameshaanza mapenzi,anamezeshwa maneno ili kumkomesha mlengwa,na rais anadaganywa ukweli wa kesi hizi kuwa ni nyingi kumbe ni za uongo,na ndio maana adhabu ni kali sana”ameleeza kwa uchungu Wakili Elizabeth Mayalla,anaefanya kazi za uwakili Visiwani Zanzibar ambae ameuomba mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kuliona suala hilo kuwa ni muhimu,kwani watu wanaonewa kwa chuki,na hawatendewi Haki.

Mmoja kati ya Mawakili wa Zanzibar akichangia suala la kubambikiwa kesi za Ubakaji.

Aidha mawakili hao pia wamelilalamikia jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar  kukaa na kesi kwa muda mrefu kwa kile kinachoitwakutokamilika kwa kwa upelelezi.Kwa mujibu wa sheria za Zanzibar,mfumo wa Upelelezi wa makosa ya Jinai unafanywa na polisi,jambo ambalo mawakili hao wamelaani kuwa ni mwanya wa rushwa na kwamba baadhi ya wazazi wanahonga polisi kuchelewesha upelelezi ili kumkomesha mhusika.

“Watu wanakaa sana Polisi kwa makosa ya uongo,tuungane mawakilitukomeshe hili,maana hata Mahakimu wamegeuka wa Zanzibar wamegeuka wanasiasa”,amesema Wakili Mwandamizi,Hassan Majogolo.

Mwanzoni mwa mwaka huu,Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilianzisha Mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za vitendo vya ubakaji,na hadi mwezi April mwaka huu (Miezi mitatu) jumla ya kesi 160 zilikuwa zimeripotiwa Mahakamani na mbili pekee zilikuwa zimeamuliwa.Adhabu ya juu ya makosa ya udhalilishaji Zanzibar hasa ubakaji na ulawili wa watoto ni hadi kifungo cha miaka 80 jela,adhabu ambayo inadaiwa kuwa ni kubwa,huku kesi nyingine zikitumia miaka mingi polisi kabla ya kufikishwa mahakamani,jambo linalodaiwa pia kuwa ukiukwaji wa Haki za binadamu kufuatia baadhi ya wahusikia katika kesi hizo wanadaiwa kusingiziwa makosa hayo ya ubakaji ili wafungwe.

Kuna Mzee mimi namfahamu kabisa,ameshtakiwa kwa ubakaji,na amekaa rock up  muda mrefu,kumbe hata hajabaka,ila watu walimtengezea kesi hiyo ili kumkomesha eti kwa sababu anajiskia sana,na anawaringia wanawake”,amesema wakili Site Habib.

Kundi jingine lililolalamikiwa na mawakili hao kuchangia ongezeko la ubabikaji wa kesi za ubakaji ni Madaktari ambao wamekuwa wakikuta mtoto tayari ameshaingiliwa kimwili,wanathibisha kuwa kweli kaingiliwa bila kuthibitisha ni nani aliyemuingilia.

“Kwa hapa Zanzibar watoto wa miaka 16 tayari washaanza mapenzi tena si mara moja,sasa kwa kumkagua tu mtoto kuwa kaingiliwa ni mkanganyiko na baadhi wanatumia nafasi hii kuumiza watu wasio na Hatia”-amemaliza wakili Zahran Yusuph,anafanya kazi zake za uwakili katika Mahakama kuu ya Zanzibar.

Wakili Site Habib

Kwa mujibu wa kanuni za adhabu za Zanzibar,anaethibitika na mahakama kuwa amefanya kosa la ubakaji,anaweza kutumikia kifungo cha kuanzia miaka 7 au kifungo cha juu cha miaka 80,ambapo kwa sasa baadhi ya majaji na mahakimu wamejikita kwenye kutoa zaidi hukumu ya miaka themani,ambayo inadaiwa kuwa hukumu katili mno hasa ikizingatiwa wengine wamesingiziwa kesi,na wengine wana umri mdogo na hivyo adhabu kuwa sawa na adhabu ya kifo maana uwezekano wa wemgine kumaliza kifungo wangali hai ni mdogo.