Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), inaendesha warsha na semina elekezi kwa viongozi wapya wa Kanda wa TLS.
Warsha hiyo ya siku mbili inayoanza leo Mei 20 itakayohitimishwa hapo kesho inafanyika katika Ukumbi wa African Dream Hotel jijini Dodoma inalenga kuwapitisha viongozi wapya wa chama hicho katika miongozo mbalimbali ya chama na kiutendaji ili kuelewa dhima ya TLS.
“Nawakaribisha sana nyote,naamini mtakuwa na nafasi nzuri ya kushiriki katika programu hii kwa ajili ya kuelewa dhima ya TLS na namna gani tutatekeleza majukumu yetu,” amesema Rais wa TLS, Dkt Edward Hosea wakati akitoa neno la ufunguzi.
Aidha kwa upande mwingine semina hiyo elekezi inahusisha mafunzo juu ya kesi za haki za binadamu na kuendesha kesi za kimkakati.Viongozi hao watapewa mafunzo kamili juu ya fursa na taratibu za kimahakama katika kutetea haki za binadamu kupitia kesi za kimkakati.
Miongoni mwa watakaotoa mafunzo hayo ni Jaji Mstaafu, Robert Makaramba na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Onesmo Olengurumwa.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA