February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

VIONGOZI WA DINI WASISITIZA UPENDO NA KWA WATU WENYE UALBINO, WAISHAURI SERIKALI MAMBO MATANO

Na: Anthony Rwekaza

Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza wametoa wito kwa Serikali kuboresha na kusimamia sheria ili ziwe madhubuti zaidi kuwalinda watu wenye ualbino, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wanaohusika kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Katika taarifa yao ambayo wameitoa Feburuari 14, 2022 kwenye vyombo vya habari na Kamati ya amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Mwanza, wameeleza kuwa wanashauri Serikali kuboresha na kusimamia sheria zinazowalinda watu wenye ualbino, huku wakishauri kuwa sheria hizo ziwe madhubuti kuwachukulia hatua kali watu watakaohusika na matendo ya ukatili.

Pia katika wito wao wameshauri kuwa zitengezwe sera rafiki zinazowapa kipaumbele Watu wenye ualbino hususani Wanawake na Watoto katika fursa mabalimbali ikiwemo elimu, ajira na mitaji ya shuguli za ujasirimali.

“Kutengeza na kusimamia sera rafiki zitakazowapa kipaumbele Watu wenye ualbino ikiwemo wakina Mama na Watoto wenye ualbino katika fursa za elimu, ajira na mitaji ya kijasiriamali” Taarifa imeeleza

Katika wito wao mwingine wameshauri kujengwa kwa kasumba ya kutoa mrejesho wa Watu wenye ualbino hususani Wanawake na Watoto amabao urudishwa kwenye jamii baada ya kutolewa kwenye maeneo yao maalumu, huku wakishauri Serikali kuwajumuhisha kwenye TASAF.

“Kutoa mrejesho wa Watu wenye ualbino hususani Wanawake na Watoto waliondoshwa kwenye maeneo maalumu na kurudishwa kwenye jamii, Serikali iwajumuishe kwenye miradi ya kuendeleza kaya maskini yaani TASAF” Taarifa imeeleza

Vilevile wametoa wito kwa Serikali kupitisha rasmu ya muongozo wa utoaji huduma elimu kwa watu wenye ualbino Tanzania, ambapo wamedai kupitishwa kwa rasimu hiyo kutasaidia kuwatengenezea mazingira jumuhishi mashuleni watu hao.

Wameongeza kuwa kuna umuhimu wa kuhamasisha wahudumu wa afya kuzingatia miongozo iliyomo kwenye mwongozo wa matibabu wa wizara ya Afya (NEMLIT na STG 2021) ihusuyo huduma za kiafaya kwa Watu wenye ualbino.

Viongozi hao wa Dini wamesema wanaamini kuwa waumini wote wanatikiwa kuheshimu binadamu wakidai jambo hilo wanalithibitisha kupitia maandiko matakatifu kuhusu maudhui ya wanadamu kuoendana, wameongeza kuwa wao kama viongozi wa Dini wanakemea aina yoyote ya unyanyapaa kwa Watu wenye ulemavu wakiwemo ualbino.

“Sisi waumini wa Dini tunaamini katika waumini wote wa dini kuheshimu binadamu, pia tunathibitisha maandiko matakatifu kuhusu kuwapenda jirani zetu pasipo ubaguzi. Tunaamini katika kukemea aina yoyote ya unyanyapaa kwa Watu wenye ulemavu, ikiwemo Watu wenye ualbino tunasisitiza kwamba waumini wa Dini zote ni binadamu wa familia moja na kwamba jambo hili ndiyo msingi wa jukumu la pamoja la kuhakikisha ustawi wa Jamii.” Taarifa imeeleza

Aidha wameongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wanatambua umuhimu wa nafasi waliyonayo ya katika jamii juu ya kuleta mabadiliko chanya ya kifkra katika jamii ya Haki na utu kwa watu wenye ualbino.

Katika taarifa hiyo wameeleza kuwa wamekuwa na ushirikiano na kufanya mazungumzo na mradi wa ‘Mothering and Albinism’ kupia chuo cha Trinity Western University kilichopo Nchini Canada.

Wameeleza kuwa mazungumzo hayo ambayo yalianza Novemba 2021 mpaka Januari 2022, ni kuwa yalijikita katika kuelimishana kuhusu hali ya ualbino na athari zake hususani kwa wanawake na watoto pamoja na nafasi ya viongozi wa Dini katika utetezi wa kundi hilo, ambapo wameongeza kuwa walipata pia fursa ya kubadilishana mawazo baina ya viongozi na viongozi wa Nje walipokutana kwenye mazungumzo.

Hata hivyo wamesema licha ya mazungumzo hayo pia wamewekeana mikakati madhubuti juu ya hatua za kuchukua wa kama viongozi kwa kutumia nafasi zao.

Pia viongozi hao wametoa rai kwa Wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapogudua vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu ikiwemo albino, huku wakisisitiza viongozi wa Dini kuendelea kudumisha amani kupitia nafasi zao ikiwemo maubili wanayotoa kwenye jamii ili kuepusha jamii na vitendo mbalimbali ikiwemo unayanyapaa na ukatili kwa watu wenye changamoto mbalimbali ikiwemo albino.

Itakumbukuwa katika miaka ya nyuma iliibuka wimbi kuripotiwa kwa matukio juu ya ukatili wa albino ikiwemo kukatwa viungo vyao, madai ya kufukuliwa kwa makabuli walipozikwa watu wenye ualbino, kunyanyapaliwa pamoja na kufanyiwa matukio mengine ya ukatili, lakini kwa mara kadhaa Sirikali ilieleza kuthibiti matukio hayo kwa kiwango kikubwa na imekuwa ikisisitiza kutowavunjia sheria watu wenye changamoto ya ualbino, hata hivyo baadhi ya matukio yamekuwa yakiripotiwa kwenye baadhi ya maeneo yanayodaiwa kuwa ni ya ukatili kwa watu hao.