February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

UVAMIZI UKRAINE: URUSI KUONDOLEWA BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU UN

Wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), leo Alhamisi, tarehe 7 Aprili 2022, wanatarajia kupiga kura kuamua kama Urusi inastahili kuondolewa katika Baraza lake la Haki za Binadamu (UNHRC), kufuatia hatua yake ya kuivamia kijeshi Ukraine.

Azimio la kuitishwa kwa kura hiyo lilitolewa na nchi ya Marekani, kufuatia mauaji ya raia wa Ukraine, katika maeneo ya Bucha, kwenye Jimbo la Kyiv.

Hata hivyo, Urusi imepinga hatua hiyo huku ikionya wanachama hao 47, KUWA wakijaribu kupiga kura ya kuiondoa UNHRC, wataonekana ni maadui wa taifa hilo.

Katika mchakato wa huo, Urusi itaondolewa kama theluthi ya wajumbe wa UN watapiga kura ya ndiyo.

Mkuu wa Urusi UN, Gennady Galitov, amesema kama nchi yake itaondolewa katika baraza hilo, itakuwa ni ukiukwaji wa kanuni za umoja huo.

“Kusimamishwa kwa haki ya Urusi kama mjumbe wa UNHRC, ni kudharau kanuni ya baraza, kuathiri ufanisi wake na kudhoofisha kabisa uaminifu, sio tu kwa haki za binadamu, lakini katika mfumo mzima wa hakiza binadamu wa UN,” amesema Gatilov.

Urusi iliivamia kijeshi Ukraine mwisho wa Februari 2022, baada ya Rais wake, Vladimir Putin, kutangaza oparesheni ya kijeshi nchini humo, ikiwa ni hatua ya kuishinikiza iache mpango wake wa kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kujihami (NATO).