Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO), na Shirika la kazi duniani (ILO) umebaini kuwa kufanya kazi kwa muda mrefu katika kipindi cha mwaka 2016, kumepelekea vifo vya watu 745,000 huku asilimia 72 ya vifo hivyo ni wanaume
Inakadiriwa kuwa watu 398,000 wamefariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi na wengine 347,000 kutokana na magonjwa ya moyo kwa mwaka huo wa 2016 na sababu kuu ikiwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu masaa 55 kwa wiki.
Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu vimeongezeka kwa asilimia 42, na kiharusi asilimia 19.Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia.
Profesa Jian Li mmoja kati wa maafisa waandamizi wa WHO, walioshiriki utafiti huo anasema wamebaini kuwa kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kunaongeza hatari ya kufa kwa asilimia 17 baada ya miaka 10 na hatari ya kupata kiharusi kwa asilimia 35 .
Hitimisho la utafiti huo linasema kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kuna hatari ya kufa mapema ikilinganishwa na kufanya kazi kwa masaa 35 hadi 40 wiki na inaelezwa kuwa idadi ya watu wanaofanya kazi kwa muda mrefu inaongezeka duniani, na kwa sasa ni asilimia 9 ya idadi jumla ya watu.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito kwa serikali, waajiri na wafanyakazi kufanya jitihada za pamoja kukukubaliana muda wa kufanya kazi ili kuzilinda afya za wafanyakazi.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS