March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“USALAMA NCHINI UNAENDELEA KUIMARIKA”-SIRRO

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wazazi pamoja na walezi kuendelea kuimarisha malezi kwa familia zao hasa katika kipindi hiki ambacho hali ya usalama nchini imeendelea kuimarika.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiwa Chalinze mkoani Pwani alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo ambapo amesema kwa sasa hakuna matukio makubwa ya uhalifu na kwamba wanaokiuka wamendelea kuchukuliwa hatua za kisheria huku akiwataka wale wanaojihusisha na uhalifu kuacha kufanya uhalifu kabla mkono wa sheria haujawafikia.

Wakati huo huo IGP Sirro pia amekagua kituo cha Polisi cha Chalinze na kuupongeza uongozi pamoja na wadau wengine werevu kwa namna walivyokiboresha kituo hicho kwa kuweka miundombinu rafiki kwa wateja wanaofika kituoni hapo kupata huduma za Kipolisi