February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

URUSI:TISA WAUAWA KATIKA SHAMBULIO SHULENI

Watu takribani tisa wameuawa kwa kupigwa risasi katika shule huko Kazan, mji ulioko katikati mwa Urusi,siku ya Jumanne hata hivyo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo wameripoti kuwa  mmoja wa washukiwa wa washambuliaji ametiwa nguvuni.

Kulingana na ripoti ya awali inaonyesha kuwa  wanafunzi wanane na mwalimu mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wengine kumi wamejeruhiwa, wanne kati yao wamelazwa hospitalini.

“Polisi walimkamata kijana, ambaye anashukiwa kuwa ndiye chanzo cha mkasa huo,” kimesema chanzo kutoka idara ya huduma ya uokoaji

Kulingana na chombo cha habari cha  Interfax na TASS cha Urusi kimeeleza kuwa mtuhumiwa wa pili anayeshukiwa kuwa na bunduki huenda bado yuko katika jengo la shule.