February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

URUSI YAJIBU MAPIGO YA MAREKANI, VIKWAZO VYATAWALA

Ikiwa zimepita saa chache tangu Serikali ya Marekani, kutangaza kuwawekea vikwazo viongozi 11 wa Ulinzi wa Urusi, nchi hiyo imejibu mapigo kwa kumuwekea vikwazo Rais wake, Joe Biden na maafisa wengine 12 wa Ikulu.

Vikwazo hivyo vimetangazwa jana Jumanne, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, ikisema hatua hiyo ni kuweka usawa kufuatia hatua ya Marekani kuwawekea vikwazo viongozi wake, ikishinikiza isitishe mapigano yake ya kijeshi nchini Ukraine.

Mbali na Biden, vikwazo hivyo pia vimewekwa kwa aliyekuwa Katibu wa Ikulu ya Marekani, Hillary Clinton.

Mtandao wa BBC Swahili, umewataja viongozi wengine wa Ikulu ya Marekani waliowekewa vikwazo, ikiwemo Katibu wa Habari, Jen Psaki. Mwenyekiti wa Wakuu wa Wafanyakazi, Mark Milley. Katibu wa Ikulu ya Marekani, Antony Blinken na Katibu wa Ulinzi, Lloyd Austin.

Vikwazo hivyo pia vinawahusu, Mshauri wa Taifa hilo wa masuala ya Usalama, Jake Sullivan na naibu wake Daleep Singh. Mismamizi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Samantha Power. Naibu Katibu wa Hazina, Wally Adeyemo na Rais wa Benki ya Export-Import ya Mrakeni, Reta Jo Lewis.

Nchi ya Urusi kwa sasa inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa, ikiwemo vya kiuchumi, kutokana na uamuzi wake wa kuivamia kijeshi Ukraine, Februari 2022.

Vita hiyo iliyoibuka tarehe 24 Februari 2022, inaendelea kurindima Ukraine, licha ya viongozi wa mataifa hiyo kufanya mazungumzo zaidi ya mara mbili bila muafaka.

Mamia ya watu wakiwemo raia na wanajeshi wa pande zote mbili, wamepoteza maisha katika vita hiyvo.