Na Loveness Muhagazi
Januari 15, kila mwaka dunia huadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mwanaharakati Mmarekani mweusi na mtetezi wa haki za binadamu aliyeongoza harakati za kupigania haki za raia Weusi, harakati zilizoleta mabadiliko ndani ya taifa ya Marekani wakati bado taifa hilo likiwa na sheria za ubaguzi wa rangi Martin Luther King Jr.
Martin Luther King Jr, Aliwaongoza Wamarekani Weusi kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwepo nchini humo hadi miaka ya 1960
Martin Luther anaheshimika kwa mbinu yake ya kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya serikali na polisi bila kutumia mabavu. Martin alitumia mbinu ya kuongoza makundi ya watu kuandamana na kuingia katika maeneo mengi yaliyotengwa kisheria maalum kwa ajili ya watu Weupe tu ikiwemo migahawa, shule na hata usafiri wa umma na kunyamaza hata walipopigwa, kukamatwa na kupewa adhabu.
Baada ya miaka kadhaa mbinu za mapambano kwa silaha hizo za amani yalishinda nah apo mahakama kuu ya Marekani na serikali kuu zilitangaza ya kuwa ubaguzi wa rangi katika mikoa mbalimbali hauruhusiwi kuendelea.
Mwaka 1964 Martin alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani iliyomtambua kuwa mtetezi wa haki za binadamu aliyetetea haki bila ya kutumia mabavu, hata hivyo aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1968, Pamoja na kifo chake mahubiri yake yalizidi kuenea maeneo mbali mbali na kupekelea sheria mbalimbali kubadilishwa.
Martin Luther amaheshimika na kukumbukwa Zaidi kwa hotuba yake inayojulikana kama “I have a dream”, aliyoitoa Agosti 28, 1963 akitaka usawa na kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi kati ya jamii zote nchini Marekani,
Watetezi TV
15 Januari, 2022
Habari Zaidi
OPEN LETTER TO HER EXCELLENCY PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSAN REGARDING LOLIONDO AND NGORONGORO SAGA
MKUTANO WA RAIS,CHADEMA KULETA MARIDHIANO YA KITAIFA?
Local residents in Ngorongoro Conservation Area oppose deliberate and systematic blockades to basic services