February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

UJERUMANI KUILIPA NAMIBIA EURO BIL. 1.1 MAUAJI YA NAMA NA HERERO KARNE YA 20.

WANAUME WA KI-HERERO WAKIWA WAMEFUNGWA MINYORORO NA WAJERUMANI KARNE YA 20.

Ujerumani imekubali kuilipa Namibia fedha kiasi cha Euro bilioni 1.1 kufadhili miradi katika jamii zilizoathiriwa na mapigano yaliyosababisha mauaji ya kimbari katika karne ya 20 baina makabila ya Nama na Herero.Serikali ya Kansela Angela Markel imefafanua kuwa fedha hizo ni sehemu ya  mapatano  na siyo fidia ya kisheria.

Makumi kwa maelfu,wanawake kwa wanaume na watoto waliuawa kwa risasi,kuteswa,na wengine wakichukuliwa hadi jangwa la Kalahari ili wafe kwa njaa chini ya vikosi vya askari wa Ujerumani kati ya mwaka 1904 na 1908 katika mapigano yaliyoongozwa na makabila ya Nama na Herero  kuupinga utawala wa kikoloni katika nchi yao,wakati ule ikijulikana kama Ujerumani ya Kusini mwa Afrika ambayo sasa ni Namibia.

Kumekuwepo na mazungumzo tangu mwaka 2015 ambayo Ujerumani umekuwa ikiyafanya na serikali ya Namibia kwa kile kilichoitwa “Kuponya Vidonda” kufuatia mauaji hayo yaliyoacha historia nchini Namibia.

Mapema Alhamisi taarifa rasmi kutoka Berlin ilitolewa na vyomba vya habari vya nchini Namibia ikieleza makubaliano yaliyofikiwa baada ya vikao nane,ambapo pande hizo mbili tayari zimekubaliana katika tamko la pamoja kuhusu malipo ya Euro bilioni 1.1 zitakazolipwa kwa Namibia nje ya misaada inayotolewa na Ujerumani kwa nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Katika fedha zitakazotolewa (Euro zaidi bilioni 1) zitakwenda kuimarisha mageuzi katika matumizi ya ardhi,miundombinu vijijini,upatikanaji na usambazaji wa maji,pamoja na mafunzo ya kuandaa wataalamu.

Kikazi cha kabila la Nama ambalo liina watu wachache zaidi katika maeneo manane yaliyoathiriwa vibaya na mapigano yale,litahusishwa pia katika kupanga mipango ya utekelezaji wa miradi iliyopewa kipaumbele.

Euro milioni 50 zitatutumika kuimarisha msingi wa mapatano baina ya nchi hizo mbili ikiwemo miradi ya kushirikishana kitamaduni,pamoja na miradi ya kubadilishana vijana kujifunza mambo mbalimbali katika nchi nyingine.

Hata hivyo Chifu wa Paramount,Vekuii Rukoro ambae ni kiongozi wa mamlaka ya kimila ya Ovaherero amekosoa  serikali ya Namibia kwa kushindwa kusisitiza fidia ya fedha.

“Siku rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir akija Nambia kujifanya kuomba msamaha,tutamzingua”,Chifu Rukoro ameviambia vyombo vya habari vya Namibia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amekaribisha makubaliano na kusema kuwa ni lengo la Ujerumani kutafuta namna ya pamoja kuelekea mapatano ya kweli kwa faida ya waathirika  wa mauaji hayo.