February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

UGANDA: WAZIRI APIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA

Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uganda na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Uganda,Jenerali Katumba Wamala  amejeruhiwa kwa kupigwa risasi  na watu wasiojulikana karibu na nyumbani kwake mjini Kampala.

Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema watu hao wenye silaha waliomshambulia Waziri huyo  walikuwa kwenye pikipiki.

Jenerali  Wamala alikuwa mkuu wa jeshi la Uganda  mwaka 2013 hadi 2017 na akapewa cheo cha waziri wa ujenzi na uchukuzi pia ni miongoni mwa wabunge 10 wanaowakilisha jeshi la Uganda  katika bunge