Rais wa Uganda,Yoweri Museveni amelaani vikali shambulizi lililofanywa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha dhidi ya Jenerali Katumba Wamala na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mtoto wa kike na dereva wa jenerali huyo.
Museveni ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa amezungumza na Jenerali Katumba takribani mara mbili na kwa sasa Katumba anaendelea vizuri na kuongeza kuwa wamepata taarifa za awali kuhusu waliotekeleza shambulio hilo.
“namtakia Jenerali Katumba afueni njema.Mlinzi wake hakupaswa kupiga risasi hewani.Alitakiwa kuwaangamiza kabisa,tungekuwa na magaidi wafu kuliko kuwatishia,”amesema Museveni huku akiwaita watu hao waliojihami kwa silaha kuwa ni nguruwe ambao hawakuthamini maisha ya wengine.
Jenerali Katumba alivamiwa hapo jana na watu waliojihami kwa silaha ambao walimiminia risasi gari lililokuwa limembeba,shambulio hilo limepelekea kifo cha mtoto wake wa kike pamoja na dereva wake huku Katumba akiachwa na Majeraha.Kwa mujibu wa taarifa zinadai kuwa shambulio hilo lilikuwa ni jaribio la kutaka kumuua Jenerali Katumba.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS