Antony Rwekaza
Kufuatia tukio milipuko miwili siku ya alhamisi Agosti, 26 2021 katika shambulio tata karibu na uwanja wa ngege wa Kabul, Nchini Afghanistan na vifo vya wanajeshi 13 wa Marekani na watu wengine wakiwemo wanawake na watoto, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali mashambulio hayo ya kigaidi.
Ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesikitishwa sana na kuuliwa bila ya hatia raia wa kawaida katika mashambulio hayo yaliyotokea Kabul, wakiwemo wanawake, watoto na vijana.
“Tunatumai serikali jumuisha itaundwa huko Kabul haraka iwezekanavyo, ili mamlaka husika zichukue jukumu la kulinda maisha na mali za Waafghani” amesema Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Wakati huohuo, kundi la kigaidi la ISIS limetangaza kuhusika na hujuma hiyo ambayo ni ya kwanza kutokea mjini Kabul tangu Rais Ashraf Ghani aitoroke nchini na mji mkuu huo wa Afghanistan kudhibitiwa na kundi la Taliban mnamo tarehe 15 Agosti.
Taarifa ya ISIS imeeleza kuwa Mwanachama wa Daesh aliyekuwa amejifunga mabomu alifanikiwa kupenya na kuufikia ummati mkubwa wa wakalimani na washiriki wa jeshi la Marekani katika kambi ya Baran karibu na Uwanja wa Ndege wa Kabul na kujiripua.
Aidha Rais wa Marekani, Joe Biden katika hotuba yake kwa taifa la Marekani, amesema kuwa zoezi la kuondoa raia wakigeni kutoka Afghanistan itaendelea licha ya shambulio lililotokea kugharimu maidha ya watu, hususan wanajeshi 13 wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Kabul, nchini Afghanistan.
Aidha kufuatia tukio hilo Joe Biden amesema kuwa kamwe Marekani haitosahau wala kusamehe mashambulio hayo, na kwamba italipiza kisasi.
“Hatutazuiliwa na magaidi Hatutawaacha wazuie operesheni yetu. Tutaendelea kna zoezi hilo” amesema Rais Joe Biden
Taarifa za awali kufuatia tukio zimeripoti kuwa Afisa mmoja wa Marekani ameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.
Ikumbukwe baada ya kundi la Talban kuvamia na kuiteka ikulu ya Afghanistan na kuibuka taharuki baada ya Rais wa Nchi hilo kukimbia, Marekani kupitia hotuba ya Rais Baden ilisikitishwa na kitendo cha Jeshi la Afghanistan licha ya kupewa mafunzo na kutoka kwenye Jeshi la Marekani kushindwa kuthibiti kundi hilo lisiteke Nchi hiyo, baada kuonyesha hivyo Marekani ilianza kuwaondoa baadhi ya raia wake na raia wengine ili kuwapa hifadhi.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS